Pata taarifa kuu
Uhispania

Maelfu wajitokeza kupiga kura Catalonia

Mamia ya watu wameanza kukusanyika katika vituo vya kupigia kura huko Catalonia nchini Uhispania mapema leo Jumapili ili kupiga kura ya kujitenga iliyopigwa marufuku na Madrid, kwa mujibu wa waandishi wa habari wa AFP katika eneo hilo.

Maelfu wakingoja mbele ya madarasa huko Barcelona kufunguliwa kwa vituo vya  uchaguzi wa kujitenga, Jumapili, Oktoba 1, 2017.
Maelfu wakingoja mbele ya madarasa huko Barcelona kufunguliwa kwa vituo vya uchaguzi wa kujitenga, Jumapili, Oktoba 1, 2017. RFI / Béatrice Leveillé
Matangazo ya kibiashara

Katika miji ya Barcelona, pamoja na Girona, ngome ya rais waCatalonia Carles Puigdemont, watu wanasema wamejitokeza mapema kabla ya aalfajiri ili kulinda vituo vya kupigia kura na kutetea haki yao ya kupiga kura, ili kuzuia jaribio la serikali kuu kuzuia uchaguzi usifanyike.

 

Hapo jana Polisi jimboni Catalonia tayarai walikuwa wamefunga zaidi ya nusu ya vituo vya kupigia kura 2,315 ili kuzuia kufanyika kwa kura ya kujitenga, serikali ya Uhispania imesema, huku wanaotaka kujitenga wakibaki na msimamo wa kuamua kupigania haki yao ya kupiga kura.

Walimu, wazazi, wanafunzi na wanaharakati katika eneo hilo tajiri la Kaskazini-mashariki wameapa kufanya lolote kutetea kura hiyo iliyopangwa kufanyika leo Jumapili, wakipuuza maonyo ya Madrid kuhusu madhara yatakayojitokeza kwa kutumia shule zaidi ya 160 zilizochaguliwa kama vituo vya kupigia kura.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.