Pata taarifa kuu
UBELGIJI-USALAMA

Meya wa Mouscron akutwa amechinjwa katika makaburi

Meya wa Mouscron, nchini Ubelgiji, alikutwa amechinjwa karibu na mpaka wa Ufaransa, Tukio hilo lilitokea siku ya Jumatatu usiku,vyombo vya habari vya Ubelgiji vimearifu.

Maafisa wa polisi Septemba 11, 2017 karibu na makaburi ya Luingne, Mouscron, ambapo meya aamekutwa amechinjwa.
Maafisa wa polisi Septemba 11, 2017 karibu na makaburi ya Luingne, Mouscron, ambapo meya aamekutwa amechinjwa. AFP
Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo imethibitishwa na mwanasheria wa Mfalme wa Mons, Christian Henry, ambaye alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa, shirika la habari la Belga limearifu.

Alfred Gadenne, mwenye umri wa miaka 71, alikutwa amekufa katika makaburi ya mji wa Mouscron karibu na nyumbani kwake, Bw Hanry amesema.

Akihojiwa na shirikala habari la AFP, Christian Hanry alikataa kutoa maelezo yoyote, akibaini kwamba anaanda mkutano na waandishi wa habari leo Jumanne.

Alfred Gadenne, kutoka chama cha CDH, alikuwa Meya wa jiji la Mouscron tangu mwaka 2006.

Wanasiasa kadhaa nchini Ubelgiji walitoa rambirambi zao kwenye Twitter, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Charles Michel.

"Ninapata taarifa kuhusu kifo cha kikatili cha Alfred Gadenne.Tutaendelea kumkumbuka kiongozi huyo mwadilifu, ameandika Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.