Pata taarifa kuu
UHISPANIA-USALAMA

Tamasha lafutiliwa mbali Rotterdam kutokana na tishio la kigaidi

Polisi ya Uholanzi waligundua gari iliyosajiliwa nchini Uhispania na ambayo ilikua imejaa mikebe ya gesi ya kutoa machozi siku ya Jumatano usiku katika mji wa Rotterdam, nchini Uholanzi, ambako kulipangiwa kufanyika tamasha la mitindo ya Rock.

Magari ya polisi karibu na ukumbi wa tamasha wa Maassilo katika eneo la bandari la Rotterdam baada ya tahadhari kwa tishio la kigaidi.
Magari ya polisi karibu na ukumbi wa tamasha wa Maassilo katika eneo la bandari la Rotterdam baada ya tahadhari kwa tishio la kigaidi. Arie Kievit / ANP / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bendi ya Allah-Las ya muziki wa Rock ilikua ilipanga kutumbwiza saa 2:30 usiku katika ukumbi wa Maasilo katika eneo la bandari kusini mwa Rotterdam. Lakini tamasha hilo lilifutiliwa mbali kabla ya kuanza kwa sababu ya "tishio la kigaidi", msimamizi wa tamasha hilo amesema kwenye Twitter.

Tamasha hili lilifutwa katika mji huu wa magharibi wa bandari wa Uholanzi, kutokana na "tishio la kigaidi," amesema meya.

Watazamaji wengi walifukuzwa na eneo hilo lilifungwa.

Taarifa hiyo imethibitishwa mara moja na polisi wa Uholanzi na meya wa jiji hilo, Ahmed Aboutaleb, ambaye tayari amesema kwa vyombo vya habari.

Hata hivyo Bw Aboutaleb amesema haijabainika iwapo gari hilo lina uhusiano na tishio la shambulio la kigaidi.

Polisi ya Uholanzi walionywa na vyombo vya usalama vya Uhispania siku ya Jumatano mchana, kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa Uholanzi.

Lakini tahadhari hiyo ya polisi wa Uhispania ilitolewa kukiwa na hali ya juu ya tahadhari baada ya mashambulio kadha kutekelezwa Uhispania wiki iliyopita.

Polisi wa Uholanzi pia wamemkamata dereva wa gari hilo kutoka Uhispania na anahojiwa.

Kikosi cha kuchunguza na kutegua mabomu kimetumwa eneo hilo, taarifa zinasema.

Polisi waliovalia fulana zisizopenya risasi wamefika eneo hilo, baada ya watu wote kuamrishwa kuondoka.

Vikosi vya usalama viligundua gari ambayo ilikuwa imeegesha karibu na ukumbi ambako kulikua kulipangwa kufanyika tamasha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.