rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uhispania Morocco UNHCR

Imechapishwa • Imehaririwa

Mamia ya wakimbizi waokolewa nchini Uhispania

media
Maafisa wa uokoaji katika Bahari ya Meditterenean REUTERS/Osman Orsal

Maafisa wa usalama na uokozi nchini Uhispania wanasema wamefanikiwa kuwaokoa wahamiaji haramu 600 waliokuwa wametokea nchini Morocco kuingia nchini humo.


Ripoti zinasema kuwa, watu hao walikuwa katika meli 15 na miongoni mwao kulikuwa na watoto 35 waliokuwa wanasafiri.

Umoja wa Mataifa unasema mwaka huu pekee, wahamiaji haramu zaidi ya 9,000 wamewasili nchini Uhispania.

Aidha, imesema kuwa idadi hii imeongezeka mara tatu ikilingalishwa na miaka iliyopita.

Hata hivyo, hadi sasa inaaminiwa kuwa watu 120 wamezama na kupoteza maisha katika Bahari ya Mediterranean.

Wakimbizi wengine hutokea barani Afrika, Syria na Yemen.

Mbali na Uhispania, nchi nyingine ya Ulaya inayoendelea kupata wakimbizi wengi ni Italia ambayo inaomba msaada ili kusaidiwa.