rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Austria Italia Wahamiaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Mvutano waibuka kati ya Italia na Austria kuhusu mgogoro wa wahamiaji

media
Idadi kubwa ya polisi wa Austria inatazamiwa kutumwa kwenye mpaka wa nchi hiyo na Italiem kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi wa Austria. GIUSEPPE CACACE / AFP

Miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa bunge nchini Austria, serikali imesema iko tayari kufunga mpaka wake na Italia. Tishio ambalo Austria tayari ilitoa mwaka jana na mwaka uliopita.


Maelfu ya wahamiaji bado wamekwama katika kati ya mpaka wa Itala na Austria, na Italia imesema inachukizwa na tabia ya majirani zake, ikiwa ni pamoja Ufaransa.

Waziri wa Ulinzi wa Austria alitangaza mjini Viena kwamba atapeleka askari kwenye mpaka na Italia ili kuzuia kuingia kwa wahamiaji wengi kutoka Italia. "Hatua hizi zitahitajika kama idadi hii kubwa ya wahamiaji haitapungua," amesema Hans Peter Doskozil. Magari manne ya kivita yamepelekwa mpakani, wakati ambapo uchaguzi wa wabunge umepangwa kufanyika nchini Austria mnamo mwezi Oktoba.

Kwa upande wa Italia, ambayo iliwapokea wahamiaji 85,000 katika miezi sita iliyopita, imesema kuwa shinikizo hili jipya la Austria halina maana. Kwanza kabisa kwa sababu idadi ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka mpaka wa Brenner imeshuka mno tangu miezi kadhaa. Jumatano hii, gazeti la kila siku la Corriere della limeendelea kuarifu kwamba mtu mmoja alikamatwa jana kwenye mpaka wa Austria.

Idadi ya wahamiaji waliowasili nchini Italia mwaka 2017 imeongezeka hadi 20% ikilinganishwa na mwaka 2016, lakini idadi ya wahamiaji wanaohpita kwenye mpaka wa Italia na Austria iko kwenye kiwango cha chini. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa jimbo la Tyrolean, wahamiaji 15 hadi 25 wanaonekana kila siku katika eneo hilo la Austria lililo kwenye mpaka na Italia.