Pata taarifa kuu
WIZI WA MTANDAO-EUROPOL

Europol: Watu zaidi ya laki 2 duniani waliathirika na uvamizi wa kwenye mtandao

Tukio la uvamizi wa kwenye mtandao lililotokea Ijumaa ya wiki iliyopita linaelezwa kuwaathiri watu zaidi ya laki mbili kwenye mataifa mbalimbali duniani, limesema shirika la polisi wasio na mipaka barani Ulaya Europol ambao wameonya kuwa huenda kukawa na matukio zaidi watu watakaporejea kazini.

Mfano wa picha ukionesha mchoro ambao sio wa uhalisia kuhusu wezi wa kwenye mtandao.
Mfano wa picha ukionesha mchoro ambao sio wa uhalisia kuhusu wezi wa kwenye mtandao. REUTERS/Kacper Pempel/Illustration
Matangazo ya kibiashara

Tayari msako wa kimataifa umeanza dhidi ya watu waliotekeleza shambulio hili la kimtandao, tuko ambalo linatajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kulenga watumiaji wa kompyuta.

Tukio hili la aina yake lilianza Ijumaa ya wiki iliyopita kwa kushambulia mabenki, hospitali na mashirika ya Serikali katika nchi zaidi ya 150, maharamia wa mtandao wakilenga kompyuta za kizamani zinazotumia programu ya mfumo wa Microsoft.

Mashirika ya Marekani ya kusafirisha vifurushi ya FedEx, kampuni ya kutengeneza magari ya Ulaya, mashirika ya simu ya Uhispania kama vile Telefonica, mfumo wa afya wa Uingereza na mtandao wa usafiri wa reli wa Ujerumano, yalikuwa ni sehemu ya yaliyoshambuliwa na uvamizi huu.

“hatujawahi kuona kitu cha aina hii,” amesema mkurugenzi wa taasisi ya sera ya Uingereza, akiliita tukio hili la “aina yake”.

“Tukio hili limeathiri watumiaji zaidi ya laki 2 karibu kwenye nchi 150, waathirika wengi wakiwa wafanyabiashara na mashrika makubwa.” imesema taarifa ya Europol.

Europol imeongeza kuwa “tuko tunakabiliwa na kitisho kitakachoendelea kwa muda mrefu”.

“Tuna hofu ya idadi ya watu watakaokuwa wameathirika wakati watu watakaporejea makazini Jumatati hii.” imesema taarifa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.