Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Raia wa Ufaransa wajiandaa kupiga kura kumchagua rais mpya

Raia wa Ufaransa kesho watapiga kura kumchagua rais katika duru ya kwanza kuelekea duru ya pili tarehe 7 mwezi Mei. 

Upigaji kura nchini Ufaransa
Upigaji kura nchini Ufaransa DR
Matangazo ya kibiashara

Ni uchaguzi unaokuja wakati huu taifa hilo likiendelea kuwa na kumbukumbu ya shambulizi la kigaidi wiki hii lililosababisha kifo cha polisi mmoja na kuwajeruhi wengine wawili jijini Paris.

Usalama umeimarishwa nchini humo hasa jijini Paris, huku polisi na wanajeshi wakionekana wakipiga doria kuhakikisha kuwa zoezi hili linkawenda vizuri.

Wachambuzi wa siasa wanaangazia uchaguzi huu kwa makini kwa sababu unakuja baada ya mabadiliko makubwa ya kisiasa duniani ikiwa ni pamoja na Donald Trump kushinda urais nchini Marekani na Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Wagombea 11 wanatafuta nafasi ya kumrithi rais Francois Hollande ambaye mwaka uliopita, alitangaza kuwa hatatetea wadhifa wake.

Licha ya Uchaguzi huo kuwa na wagombea wengi, watano ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

Watano hao ni pamoja na François Fillon kutoka chama cha Les Republicains, Benoît Hamon kutoka chama cha Kisosholisti, Marine Le Pen kutoka mrengo wa Front National, Emmanuel Macron ambaye ni mgombea binafsi na Jean-Luc Mélenchon kutoka chama cha La France insoumise.

Hata hivyo, wachambuzi nchini humo wanasema kuwa Marine Le Pen na Emmanuel Macron huenda wakamaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili na kumenyana katika mzunguko wa pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.