Pata taarifa kuu
NEW ZEALAND-SIASA

Waziri Mkuu wa New Zealand John Key ajiuzulu

Waziri Mkuu wa New Zealand John Key ametangaza kwamba atajiuzulu wadhifa wake baada ya kuhudumu kwa miaka minane, akisema kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na sababu za kifamilia.

John Key, Waziri Mkuu wa New Zealand wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Auckland tarehe 9 Novemba, 2008.
John Key, Waziri Mkuu wa New Zealand wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Auckland tarehe 9 Novemba, 2008. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia uamuzi huo, Makamu Waziri Mkuu Bill English anatarajiwa kuchukua majukumu ya uwaziri mkuu hadi chama cha National Party kikutane na kumteua Waziri Mkuu mpya.

John Key alitangaza kujiuzulu kwake kwenye kikao cha wanahabari cha kila wiki, ambapo alisema uamuzi wake umetokana na sababu za kifamilia.
Alisema huo ndio uamuzi mgumu zaidi ambao amewahi kuufanya maishani. "Sijui nitafanya nini baada ya hapa," Bw Key amesema.

Bw Key, ambaye zamani alifanya kazi Merrill Lynch kama mfanyabiashara wa sarafu za kigeni, alifikisha kikomo utawala wa Chama ch leba mwaka 2008 alipomshinda Helen Clark.

Alichaguliwa kwa muhula wa tatu kupitia chama cha National Party Septemba 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.