Pata taarifa kuu
ARMENIA-OIF

Armenia yateuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa OIF mwaka 2018

Marais na viongozi wa serikali ishirini walioshiriki katika mkutano wa kilele wa nchi zinazozungumza Kifaransa uliofanyika katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo, wameiteua nchi ya Armenia kama mwenyeji wa mkutano ujao wa OIF utakaofanyika mwaka 2018. Kwa upande wake, Tunisia itakuwa mwenyeji wa mkutano wa OIF mwaka 2020.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau miongoni mwa wakuu wa nchi na Serikali waliokuwepo katika mkutano wa kumi na sita ya Francophonie.
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau miongoni mwa wakuu wa nchi na Serikali waliokuwepo katika mkutano wa kumi na sita ya Francophonie. GIANLUIGI GUERCIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati ambapo mkutano wa kumi na sita wa Francophonie ukimalizika Jumapili jioni Novemba 27, wakuu wa nchi na serikali walikubali kuiteua nchi ya Armenia kama mwenyeji wa mkutano ujao wa jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) mwaka 2018. Tunisia, ambayo ilikuwa katika mbio za kuwania kuwa mwenyeji wa mkutano wa jumuiya hiyo mwaka 2018, imefanikia kuteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa OIF mwaka 2020.

Mkutano huu wa Antananarivo ulikua na ushiriki mdogo wa Wakuu wa nchi na serikali ikilinganishwa na ule uliofanyika mjini Dakar, nchini Senegal. Marais kumi na tatu Mawaziri Wakuu saba ndio walioshirii mkutano huo wakati ambapo katika mkutano uliofanyika mjini Dakar, nchini Senegal na Marais 23, Wakamu wa rais wawili na Mawaziri Wakuu wanane walishiriki mkutano huo.

Mwaka huu, nchi tano zimewasilisha maombi yao kujiunga katika jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF), lakini nne pekee zimekubaliwa. Nchi hizo ni pamoja na Korea Kusini, Argentina na New Caledonia na Ontario.

Le centre de conférences d'Antananarivo où a lieu le 16e sommet de la Francophonie ce week-end.
Le centre de conférences d'Antananarivo où a lieu le 16e sommet de la Francophonie ce week-end. GIANLUIGI GUERCIA / AFP

Hata hivyo, Saudi Arabia haikukubaliwa ombi lake kutokana na kwamba faili yake haikamiliki. Ombi la Saudi Arabia kujiunga katika jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa limeahirishwa kwa mkutano wa kilele ujao mwaka 2018 na ombi hilo litajadiliwa kabla kufanyiwa uchunguzi na jopo la OIF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.