Pata taarifa kuu
POLAND-HAKI

Wanawake wamiminika mitaani nchini Poland

Wanawake mia kadhaa wameandamana Jumatatu hii katika miji ya Poland kwa kupinga mpango wa serikali ya Conservative ya kuzuia haki ya utoaji mimba.

Wanawake wakibeba mabango ambayo yaliandikwa "maelewano kuhusu utoaji mimba yanaua" na "marufuku yautoaji mimba yanaua" mbele ya kanisa katika mji wa Warsaw.
Wanawake wakibeba mabango ambayo yaliandikwa "maelewano kuhusu utoaji mimba yanaua" na "marufuku yautoaji mimba yanaua" mbele ya kanisa katika mji wa Warsaw. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wanawake hao wamekua wakisikia kauli ya Jaroslaw Kaczynski, kiongozi wa chama tawala cha Kihafidhina cha PiS , ambapo alipiga marufuku utoaji mimba katika matukio ya watoto wenye upungufu mkubwa wa viungo vyao vya mwili, ili waweze kuzaliwa na kuzikwa kwa desturi ya kimila.

Televisheni mbalimbali zilionyesha mamia ya wanawake wakivaa nguo nyeusi, wakiandamana katika mitaa ya miji mikubwa kama vile Warsaw, Katowice, Wroclaw, Poznan, Gdansk na Bialystok.

Maandamano haya mapya yaliandaliwa na kundi liitwalo 'Mgomo wa Kitaifa wa Wanawake' na kuendeshwa dhidi ya sera ya serikali ya PiS na dhidi ya mshirika wake, kanisa la Kikatoliki lenye ushawishi mkubwa nchini Poland.

"Sitaki Bw Kaczynski na Kanisa kuchukua maamuzi kuhusu maisha yangu," amesema mwanamke mwenye umri wa miaka 34, ambaye aliandamana Jumatatu hii katika mitaa ya mji wa Warsaw.

Tarehe 6 Oktoba, bunge la Poland lilikataa rasimu ya awali ya serikali inayopiga marufuku utoaji mimba. Siku tatu baadaye, maelfu ya wanawake, kwa mshangao wa Wabunge, waliingia mitaani ili kupinga "maandamano meusi" dhidi ya rasimu hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.