Pata taarifa kuu

Papa Francis afanya ziara ya kiishara katika kambi ya Auschwitz-Birkenau

Siku ya tatu ya ziara yake ya Utume katika mji wa Krakow ikiwa n siku ya Siku ya Vijana Duniani, Papa Francis, Ijumaa hii Julai 29 asubuhi, atazuru kambi ya Auschwitz-Birkenau. Ziara ambayo inaonekana tofauti na zile za watangulizi wake.

Papa Francis, wakati wa Siku ya Vijana Duniani (WYD), Julai 28, 2016 katika mji wa Krakow.
Papa Francis, wakati wa Siku ya Vijana Duniani (WYD), Julai 28, 2016 katika mji wa Krakow. REUTERS/Kacper Pempel
Matangazo ya kibiashara

Mwaka 1979 Papa John Paul II aliongoza misa katika kambi hiyo, mwaka 2006, Papa Benedict XVI alitoa hotuba mbele ya waumini waliokua wamezuru kambi hiyo ya mateso na ukatili, wote wawili walifanya maombi makubwa katika eneo hili ambalo ni mfano wa ugaidi wa utawala wa kiimla.

Lakini ziara hizi zilizua utata. Papa John Paul II, alishtumiwa wakati huo kuwa alitaka kufanya kambi hiyo kuwa ya Wakristo wakati ambapo wengi walioangamia ni Wayahudi. Nae Benedict XVI alishtumiwa alipuuzia vikali katika hotuba yakewajibu wa raia wa Ujerumani ikilinganishwa na utawala wa kiimla.

Pamoja na Papa Francis, ziara hii itakuwa tofauti. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki dunianisi raia wa Poland wala Ujerumani lakini ni raia wa Argentina, yaani mbali kabisa tukio hilo la kughadhabisha lililotokea Ulaya. Aidha, kama alivyosema hivi karibuni, "anataka kuzuru nafasi hii ya kutisha bila hotuba au kushindikizwa na mtu yeyote."

Vijana Wakatoliki wakikutana na Papa Francis katika mji wa Krakow Julai 28, 2016.
Vijana Wakatoliki wakikutana na Papa Francis katika mji wa Krakow Julai 28, 2016. REUTERS/Kacper Pempel

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.