rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

EU Ujerumani Uingereza David Cameron Barack Obama

Imechapishwa • Imehaririwa

Scotland: Tutafanya kura yetu ya maoni, sahihi milioni 1 zapatikana

media
Waziri wa mambo ya nje wa Italia, Paolo Gentilon na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, wakiteta kando na mkutano wao wa hapo jana mjini Berlin. REUTERS/Axel Schmidt

Waziri wa kwanza wa Scotland, Nicola Sturgeon, amesema ataomba kufanyika haraka kwa mjadala na wakuu wa Brussels ili kuilinda nchi yake kwenye mkataba wa umoja wa Ulaya, baada ya nchi ya Uingereza kupiga kura ya kuachana na jumuiya hiyo.


Akizungumza punde baada ya kumalizika kwa mkutano wa dharura wa baraza lake la mawaziri, Sturgeon amesema, wamekubaliana kuomba mjadala wa dharura na taasisi za umoja huo pamoja na nchi nyingine wanachama, kuangalia uwezekano wa nchi yake kulindwa na kupewa nafasi ndani ya umoja wa Ulaya.

Nchi ya Uingereza kwa ujumla imepiga kura kwa asilimia 52 kwa asilimia 48 kuondoka kwenye jumuiya ya Ulaya, katika tukio la kihistoria la kura ya maoni nchini humo. Lakini Scotland ilipiga kura kwa nguvu Uingereza kusalia kwenye umoja wa Ulaya kwa asilimia 62 dhidi ya 38.

Siku ya Ijumaa, Sturgeon alisema kuwa matokeo ya kura ya maoni Uingereza kujitoa kwenye umoja wa Ulaya, yametoa nafasi ya kufanyika upya kwa kura ya maoni kutaka uhuru wa Scotland, na kwamba huenda kura hiyo ikafanyika ndani ya miaka miwili ijayo.