Pata taarifa kuu

Idadi ya wakimbizi wanaowasili Ugiriki yashuka kwa kasi

Baada ya idadi ya wahamiaji waliowasili nchini Ugiriki mwezi Aprili kushuka kwa 90 %, kutangazwa Ijumaa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), polisi ya Ugiriki imesema kuwa hakuna mkimbizi aliyeripotiwa kuwasili tangu Jumamosi katika visiwa vya nchi hiyo.

Frontex, shirika linalojihusisha na ulinzi wa mipaka ya nje ya EU, linathibitisha kwamba idadi ya wakimbizi walioowasili Ugiriki mwezi Aprili imepungua  kwa 90%.
Frontex, shirika linalojihusisha na ulinzi wa mipaka ya nje ya EU, linathibitisha kwamba idadi ya wakimbizi walioowasili Ugiriki mwezi Aprili imepungua kwa 90%. REUTERS/Darrin Zammit
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano kati ya Brussels na Ankara yaliyoafikiwa ili kupunguza wimbi la wahamiaji barani Ulaya yanaonekana kuza matunda. Inabidi hata hivyo kuwa waangalifu. Kwa uhakika, hakuna mkimbizi wowote aliyewasili katika visiwa vya Ugiriki mwishoni mwa wiki hii, lakini wahamiaji hamsini na saba walioingia Ugiriki wakipipitia kwenye mpaka wa nchi hiyo na Uturuki walikamatwa kaskazini mwa nchi, karibu na eneo la Thessaloniki.

Waliweza kuvuka mpaka wa nchi kavu na Uturuki katika mto wa Evros baada ya kulipa Euro 3,000 kila mmoja, mwandishi wetu katika mji wa Athens, Charlotte Stiévenard amearifu. Tangu ujenzi wa uzio wa kilomita 12 kando ya mto mapema mwaka 2012, barabara hii ilikuwa haitumiwu tena. Lakini polisi wa Ugiriki wameshuhudia kwa mara nyingine tena watu wakianza kuitumia.

Tangu kufungwa kwa barabara inayoelekea katika nchi za Balkan pamoja na makubaliano na Uturuki idadi kubwa ya wakimbizi waliokua wakiingia Uturuki imepungua, lakini sasa Italia ina hofu kuwa huenda sehemu moja ya wakimbizi hao wakiingia katika ardhi yake. Mwezi Aprili, walikuwa wengi kupitia nchini Itali kuliko Ugiriki. Ni mara ya kwanza hali hii inatokea tangu mwezi Juni 2015 kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi na shirika la FRONTEX, mwandishi wetu amearifu. mabadiliko ambayo huenda yasidumu, kwa sababu nchi za Ulaya zinachelewa kutekeleza masharti yaliyotolewa naUturuki ifikapo mwezi Juni. Msamaha wa viza kwa raia wa Uturuki wanaokwenda Ulaya.

Kwa upande wake msemaji wa shirika la Ulaya linalojihusisha na ulinzi wa mipaka (FRONTEX), Eva Moncure, amesema hali hii ya kupungua kwa wakimbizi ni ya muda. "Ni lazima kuzingatia muda mrefu, kwa sababu hali ya hewa ni moja ya changamoto ya hali hii, " ameonya. "Wiki mbili ya hali mbaya ya hewa inatosha kushuhudia kupungua kwa wakimbizi wanaingia Ugiriki. Hii haimaanishi kwamba kutakuwa na ongezeko kubwa la wakimbizi wakati hali ya hewa itakua nzuri. Ni kuangalia hali hii kwa muda mrefu, na wala sio kipindi kifup. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.