rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Norway

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 13 wakisiwa kupoteza maisha katika ajali ya helikopta

media
Maafisa wa Idara za huduma za dharura wakiendelea na shughuli ya uokoaji katika eneo la ajali karibu na Bergen, Norway. REUTERS/Scanpix/Marit Hommedal

Watu 13 waliokua katika helikopta iliyoanguka katika pwani ya magharibi mwa Norway Ijumaa hii wanasadikiwa kuwa wamepoteza maisha, polisi ya nchi hiyo imetangaza katika magazeti mawili ya kila siku ya AFTENPOSTEN na VG.


Mamlaka ya safari za ndege nchini Norway, imechukua hatua za tahadhari ya kawaida, kupiga marufuku safari za helikopta aiana ya H225 Super Puma, muundo wa helikopta iliyofanya ajali.

“Watu wote waliokua ndani ya helikopta wanakisiwa kuwa wamefariki” amesema mratibu wa operesheni za polisi akinukuliwa na magazeti hayo mawili.

Mashahidi wanasema wameona kifaa cha injini ya helikopta kikidondoka kabla ya ajali hiyo, kwa mujibu wa vyombo vy habari vya Norway.