Pata taarifa kuu
UN-UGIRIKI-AJALI

Watu wengi wakufa maji katika bahari ya Mediterranean

Umoja wa Mataifa unasema umetuma ujumbe wake nchini Ugiriki kuchunguza ripoti za kuzama kwa mamia ya watu katika Bahari ya Mediterranean.

Mamia ya watu hawajulikani walipo baada ya boti yao kuzama katika bahari ya Mediterranean.
Mamia ya watu hawajulikani walipo baada ya boti yao kuzama katika bahari ya Mediterranean. REUTERS/Giorgos Moutafis
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa huenda kati ya wahamiaji 400 na 500 wamepoteza maisha baada ya kuzama katika Bahari hiyo.

Uchunguzi huu umetangazwa ma msemaji wa Shirika la wakibizi duniani, Ariane Rummery, baada ya kuzuka kwa ripoti hizo kutoka kwa Mashirika yasiyokuwa ya serikali.

Inaelezwa kuwa miongoni mwa wakimbizi hao walikuwa raia wa Somalia waliokuwa wanakwenda Ugiriki ili kupata nafasi ya kwenda kuishi barani Ulaya.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi (UNHCR) limesema wakimbizi hao walikuwa wametokea nchini Misri na kukutana na wengine waliokuwa wametoka nchini Libya, waliohamia katika boti lililokuwa limetokea nchini Misri kabla ya kuzama baharini.

Manusura 37 wakiume, wanawake watati na mtoto wa miaka mitatu wamepatikana baada ya kuzama kwa boti hiyo.

Sio mara ya kwanza mkasa kama huu kushuhudiwa katika Bahari ya Mediterranean.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.