Pata taarifa kuu
UGIRIKI-MAKEDONIA-WAKIMBIZI

Wahamiaji wafukuzwa kutoka Makedonia

Ulaya inaonekana kuwa imefunga mipaka yake: barabara inayoelekea katika nchi za Balkan, ambayo imekua ikitumiwa mpaka sasa na maelfu ya wahamiaji wanaokimbia vita nchini Syria, Iraq na Afghanistan, imefungwa kwa wiki kadhaa sasa.

Alexis Tsipras amewatolea wito wakimbizi 12 000 wanaokusanyika katika mji wa Idomeni kwenye mpaka kati ya Ugiriki na Makedonia kuchukua hatua ya kurejea katika vituo tofauti viliotengwa nchini Ugiriki.
Alexis Tsipras amewatolea wito wakimbizi 12 000 wanaokusanyika katika mji wa Idomeni kwenye mpaka kati ya Ugiriki na Makedonia kuchukua hatua ya kurejea katika vituo tofauti viliotengwa nchini Ugiriki. REUTERS/Sasa Kavic
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu Machi 14, baadhi ya wakimbizi 1,500 waliokua wamezuiliwa nchini Ugiriki waliweza kuingia kwa nguvu Makedonia. Lakini Jumanne hii walihamishwa hadi katika kambi ya Idomeni nchini Ugiriki. Uamuzi ambao umeishangaza serikali ya Athens.

Makedonia imefanya uamuzi wake bila kuzishirikisha au kuzitaarifu nchi jiranikama Ugiriki, mamlaka ya Makedoniaimewafukuza wahamiaji 1500 walioingia katika ardhi yake kinyume cha sheria. Jeshi la Makedonia liliunda makundi madogo ya wakimbizi, na kuyasafirisha katika malori hadi kwenye mpaka na Ugiriki. Mamia ya wahamiaji wamevuka na kurudi kwenye kambi yao ya Idomeni, nchini Ugiriki.

Nchini Ugiriki, uchunguzi umeanzishwa lakini kwa kusubiri barabara ya kuelekea katika nchi za Balkanitaendelea kufungwa, amesema Waziri Mkuu wa Ugiriki. Kama suluhu, Alexis Tsipras amewatolea wito wakimbizi 12,000 wanaokusanyika katika mji wa Idomeni kwenye mpaka kati ya Ugiriki na Makedonia kuchukua hatua ya kurejea katika vituo tofauti viliotengwa nchini Ugiriki.

Hali ni ya kutisha katika kambi ya Idomeni, amesema upande wake Kamishna wa wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya Uhamiaji, ambaye anatembelea kambi hiyoi. Lakini anaona kuwa suluhisho pekee ni kufuata njia 'halali'ya kugawana wakimbizi katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.