Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UGIRIKI-WAKIMBIZI

Wahamiaji: Merkel aitahadhari EU kuhusu ongezeko la wahamiaji Ugiriki

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameutahadhari Umoja wa Ulaya kufuatia suala la wahamiaji ambao wameendelea kuongezeka kwa idadi kubwa nchini Ugiriki.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel. REUTERS/Hannibal Hanschke
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya hauwezi kuaiacha Ugiriki katika 'hali ya sintofahamu" dhidi ya ongezeko la wakimbizi, amesema Jumapili hii Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, baada ya mipaka ya ncho za Balkan kufungwa.

Ugiriki ilionya kuwa idadi ya wahamiaji wanaozuiliwa katika ardhi yakeinaweza kuongezeka mara tatu mwezi Machi, kufikia idadi ya watu 70,000 kutokana na idadi iliyolazimishwa na nchi za Balkan kwa wakimbizi au wahamiaji wanaoomba hifadhi katika nchi za Ulaya ya Magharibi.

"mnaweza kuamini kwa umakini kwamba nchi (eneo) la nchini zitazotumia sarafu ya Euro zilipambana kwa nguvu zao zote ili Ugiriki ibaki katika eneo la nchi zinazotumia sarafu ya euro (...) kwa mwaka mmoja baadaye, Ugiriki inaachwa iendelee kukabiliwa hali kama hii, je hii ni sahihi?", Angela Merkel amesema wakati wa mahojiano yaliorushwa hewani kwenye runinga ya serikali ya ARD.

"Wajibu wangu ni kwamba Ulaya inatakiwa kutafuta njia ikiwa pamoja," ameongeza Merkel, akisisitiza kwamba anawasiliana mara kwa mara na Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras.

"Kulingana na makadirio yetu, idadi ya wale ambao watakabiliwa na hali ngumu nchini mwetu wanafikia kati ya watu 50,000 na 70,000 kwa mwezi ujao," Waziri wa Sera za Uhamiaji wa Ugiriki, Yiannis Mouzalas, alisema hivi karibuni. "Leo hii, kuna watu 22,000 wakimbizi na wahamiaji" nchini Ugiriki alisema katika mahojiano yaliorushwa hewani kwenye runinga ya Mega.

Karibu watu 6,500 kati yao walikuwa wamekwama Jumapili hii katika kambi ya muda karibu na kijiji cha Idomeni, kaskazini mwa Ugiriki, kwenye mpaka na Makedonia. Baadhi 500 wengine walikuwa wamewekwa katika kituo cha mafuta, kilomita12 na kijiji cha Idomeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.