Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-KUSIMAMISHWA

Soka: Platini na Blatter wasimamishwa

Sepp Blatter, rais wa zamani wa Shirikisho la soka duniani FIFA, pamoja na naibu wake Michel Platini,  rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA wamepigwa marufuku ya kutoshiriki katika maswala ya soka kwa kipindi cha miaka minane.

Mswisi Joseph Blatter (kushoto) na Mfaransa Michel Platini.
Mswisi Joseph Blatter (kushoto) na Mfaransa Michel Platini. REUTERS/Ruben Sprich/Files TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukuliwa na Majaji wa Jopo maalum lililokuwa linachunguza tuhuma za ufisadi dhidi ya wawili hao, na Jumatatu hii Desemba 21 Jopo hilo limefikia maamuzi kuwa Blatter na Platini walihusika na ufisadi.

Blatter amekuwa akituhumiwa kumlipa Platini Dola za Marekani Milioni 2 malipo ambayo hayakufanywa kwa njia sahihi kwa mujibu wa kamati ya maadili ya FIFA.

Pamoja na adhabu hiyo, Blatter ambaye amekuwa akiongoza FIFA tangu mwaka 1998 ametozwa faini ya Dola 50,000 huku Platini akitozwa Dola 80,000.

Blatter na Platini wameendelea kusisitiza kuwa malipo hayo yaliyofanyika mwaka 2011 yalikuwa makubaliano ya watu wawili, baada ya Platini kufanya kazi ya kumshauri Blatter kuhusu maswala mbalimbali ya soka.

Majaji wa Jopo hilo pia wamewapata wawili hao na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na hatua hii inaamanisha kuwa Blatter mwenye umri wa miaka 79, huu ndio mwisho wake kujihusisha na maswala ya soka.

Platini mwenye umri wa miaka 60 ndoto yake ya kuchukua nafasi ya Blatter imedidimia kuelekea uchaguzi utakaofanyika mwezi Februari mwaka ujao.

Wawili hao wanaweza kukata rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo kupinga adhabu ya Jopo hilo.

Blatter amesema atakata rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo dhidi ya uamuzi huo na ameongeza kuwa ameonewa na Jopo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.