Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-UFISADI

Sepp Blatter mbele ya majaji wa FIFA

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA aliyesimamishwa kazi kwa siku 90 kwa tuhma za ufisadi Sepp Baltter amefika mbele ya Majaji wa Kamati ya maadili ya Shirikisho hilo jijini Zurich nchini Uswisi.

Rais wa UEFA Michel Platini (kulia) na rais wa FIFA Sepp Blatter baada ya kuchaguliwa kwa Blatter kulingoza Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), Zurich, Mei 29, 2015.
Rais wa UEFA Michel Platini (kulia) na rais wa FIFA Sepp Blatter baada ya kuchaguliwa kwa Blatter kulingoza Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), Zurich, Mei 29, 2015. REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Blatter ambaye aliambatana na wakili wake hakuwaambia wanahabari lolote wakati akiingia katika chumba cha mahojiano.

Kabla ya kuhojiwa na Kamati hiyo, Blatter aliyaandikia barua mashirikisho yote ya soka duniani kukosa imani na wajumbe wa Kamati hiyo ya maadili.

Blatter mwenye umri wa miaka 79 amekuwa akikanusha madai ya kuhusika na tuhma za rushwa katika Shirikisho hilo aliloliongoza tangu mwaka 1998.

Pamoja na Blatter, Michel Platini rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya anayetuhumiwa kulipwa Dola Milioni 2 na Blatter amesema hatofika mbele ya kamati hiyo siku ya Ijumaa badala yake atamtuma wakili wake.

Wawili hao wamekanusha kuhusika na tuhma za ufisadi na ikiwa watapatikana na kosa, huenda wakafungiwa kushiriki katika maswala ya soka kwa muda wa miaka saba.

Wakati hayo yakijiri, rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Blatter anastahili kushinda tuzo ya amani ya Nobel kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya katika Shirikisho la la FIFA.

Urusi itakuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018 na rais Putin amekuwa akiyashtumu mataifa ya Magharibi kwa kumlenga Bwana Blatter kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.