Pata taarifa kuu
UBELGIJI-USALAMA-UGAIDI

Brussels yazingirwa kufuatia tishio la mashambulizi ya kigaidi

Mji wa Brussels utakua tena katika "tahadhari" Jumatatu hii, ukizingirwa na jeshi. Hali ya sintofahamu imeendelea kushuhudiwa katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels na katika miji mji mikuu barani Ulaya ambapo wahusika wa mashambulizi yaliotokea usiku wa Novemba 13 jini Paris wanaendelea kusakwa.

Polisi yatenga eneo la usalama  katika mji wa Brussels, Novemba 22, 2015.
Polisi yatenga eneo la usalama katika mji wa Brussels, Novemba 22, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumapili usiku, kulifanyika operesheni nyingi za polisi, hasa katikati mwa mji wa Brussels, karibu na eneo la Grand-Place, ambapo kwa mujibu wa mpiga picha wa shirika la habari la Ufaransa la AFP eneo la usalama limetengwa na katika mkoa wa Charleroi,kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Ubelgiji.

Chanzo kilio karibu na viongozi wa Ubelgiji kimebaini pia kuwa msako ulioendeshwa katika mji wa Brussels na viunga vyake umepomaliza, kabla mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya mashtaka ya Ubelgiji. Mkutano ambao ullikua ukisubiriwa kufanyika usiku wa manane.

Polisi imeomba vyombo vya habari kutopeperusha hewani taarifa kuhusu operesheni itakayofanyika na mazingira ya eneo lenyewe, na kujiepusha kupeperusha hewani moja kwa moja picha za operesheni wakati itakua ikiendeshwa.

Tishio kwa mji mkuu wa Ubelgiji linachukuliwa kama "lipo tena kubwa" wakati ambapo polisi bado inaendelea kumsaka mtuhumiwa mkuu katika mashambulizi yaliotokea Novemba 13 jijini Paris, Abdeslam Salah, na kuwashuku watu wengine kutaka kuendesha vitendo vya kigaidi.

Baada ya kushauriana na vyombo vya usalama, uamuzi wa kuendelea na hali ya tahadhari ya ugaidi katika kiwango cha juu umechukuliwa katika mkoa wa Brussels (wenye wakazi milioni 1.2) na "kupunguza matukio makubwa (kama sherehe), kuendelea kufungwa kwa vituo vya treni za mwendo kasi ", Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel , ametangaza Jumapili hii jioni.

"Shule zitafungwa Jumatatu hii mjini Brussels na vitalu, vyuo vikuu na shule za sekondari", Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel ameongeza. Ni ,ara ya kwanza hali hii kushuhudiwa nchini Ubelgiji. Tathmini mpya ya kiwango cha tahadhari itafanyika Jumatatu mchana wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.