Pata taarifa kuu
SLOVENIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Slovenia yakabiliwa na ongezeko la wahamiaji

Slovenia, moja ya nchi ndogo za Ulaya, inakabiliwa na mgogoro wa wahamiaji, baada ya kuzidiwa na "wingi" wa maelfu ya wahamiaji wanaotokea katika nchi za Balkan, huku wengi wao wakionekana wamechoka.

Wahamiaji wakisubiri kuingia Slovenia, Oktoba 19, 2015,Trnovec.
Wahamiaji wakisubiri kuingia Slovenia, Oktoba 19, 2015,Trnovec. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati wibi la wahamiaji wanaotafuta hifadhi wameendelea kuelekea Uturuki.

Hali ni tete na huenda ikaenea katika ncha mbili za barabara zinazotokea katika nchi za Balkan inayoingia Ulaya Magharibi. Wanaume, wanawake na watoto, ikiwa ni pamoja na raia wa Syria, Afghanistan na Iraq waliokimbia vita, wameendelea kuingia katika nchi ya Slovenia. Ugiriki inakabiliwa siku za hivi karibuni na " wimbi la wahamiaji ," kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi (HCR), wakati ambapo Slovenia ikisema kuzidiwa na wingi wa wahamiaji kwenye mipaka yake.

Serikali ya Slovenia, ambayo imebaini kwamba wahamiaji 19,500 waliingia katika ardhi yake tangu Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita, imetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuisaidia. Slovenia tangu majira ya Joto imekua ikijaribu kukabiliana na hali hii isiyokuwa ya kawaida lakini inashindwa kupata ufumbuzi.

Baada ya Hungary kufunga mpaka wake na Croatia, wahamiaji sasa wanapitia katika nchi hii ndogo yenye wakazi milioni mbili ambayo imeamua kupanua madaraka ya jeshi kwa aina ya kipekee.

" Wingi wa wahamiaji katika siku tatu zilizopita inazidi uwezo wetu ", serikali imeonya, na kuhakikisha hata hivyo kuwa matumizi ya jeshi " haimanishi hali ya hatari."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.