Pata taarifa kuu
URUSI-SYRIA-UKRAINE-VIKWAZO-USHIRIKIANO

Ukraine: mazungumzo ya amani katika kivuli cha mgogoro wa Syria

Viongozi wa Ufaransa, Urusi, Ujerumani na Ukraini wanakutana Ijumaa wiki hii katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, kuimarisha amani nchini Ukraine, na kuna uwezekano Urusi iondolewe vikwazo vinayoikabili.

Kutoka kulia kwenda kushoto, Kansela Angela Merkel, Rais wa Urusi Vladimir Putin, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko na Rais wa Ufaransa, François Hollande, Oktoba 2, 2015 jijini Paris kujaribu kuendeleza amani nchini Ukraine.
Kutoka kulia kwenda kushoto, Kansela Angela Merkel, Rais wa Urusi Vladimir Putin, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko na Rais wa Ufaransa, François Hollande, Oktoba 2, 2015 jijini Paris kujaribu kuendeleza amani nchini Ukraine. AFP/KREMLIN POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa urusi imejikita na mgogoro unaoendelea nchini Syria, baada ya kuanzisha mashambulizi ya nga dhidi ya kile viongozi wa Urusi wanachosema ni vita dhidi ya magaidi.

" Muda unayoyoma. tunapaswa kufanya kazi kwa kiwango cha juu, kuboresha mazingira tukiwa sote pamoja kwa kujaribu kuondoa vikwazo", kwa utekelezaji wa makubaliano ya pili ya Minsk ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba, chanzo cha kidiplomasia cha Ufaransa kimeeleza.

Mikataba hiyo, iliyoafikiwa kati ya wahusika wakuu Februari 12 katika mji mkuu wa Belarusi katika usiku wa mazungumzo, inalenga kumaliza mgogoro kati ya waasi wanaounga mkono Urusi katika na jeshi la Ukraini. Machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu 8,000 Mashariki mwa Ukraini tangu Aprili mwaka 2014.

Wakati wa mkutano huu, rais hollande amekubali mwaliko wa kuitembelea Ukraine, kwa mujibu wa mtandao wa Ofisi ya Rais wa Ukraine. Viongozi hao wawili wamejadili hali inayoendelea katika mkoa wa viwanda wa Donbass lakini pia katika peninsula ya Crimea iliyoonganishwa na Urusi mwaka uliyopita.

Tangu mkutano wao wa kwanza Juni 6 mwaka 2014 katika mji wa Normandie (Ufaransa) kujaribu kutatua mgogoro uliyosababisha mvutano mkali kati ya urusi na nchi za Magharibi tangu vita baridi, viongozi hao wanne walikuwa tayari kukutana mara mbili katika kikao kama hiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.