Pata taarifa kuu
AUSTRIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji waendelea kuingia Ulaya, na wengine kukabiliwa na ajali

Baada ya safari ngumu kupitia Balkan Magharibi, wahamiaji wameendelea kuwasili kwa maelfu Jumapili nchini Austria, wakati wengine wamepoteza maisha tangu mwanzo wa safari hii wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean.

Polisi ya Hungary ikwasindikiza wahamiaji waliovuka mpaka wa Croatia, Septemba 20, 2015, katika mji wa Zákány, nchini Hungary.
Polisi ya Hungary ikwasindikiza wahamiaji waliovuka mpaka wa Croatia, Septemba 20, 2015, katika mji wa Zákány, nchini Hungary. Jure Makovec/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la Visegrad (Poland, Jamhuri ya Czech, Slovakia na Hungary) watakutana siku ya Jumatatu katika mji wa Prague na mwenzao wa Luxemburg Jean Asselborn, ambaye kwa sasa nchi yake ni mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya, kuzungumza kuhusu suala hili na mgogoro wa uhamiaji, mgogoro mkubwa kuwahi kulikumba bara la Ulaya tangu mwisho wa Vita vikuu vya II vya dunia.

Mawaziri wa wa mambo ya nje wa Romania pia atahudhiria mkutano huo.

Na Jumanne wiki hii Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja watakutana, siku moja kabla ya mkutano wa kilele mjini Brussels ili kujaribu kuweka kando mgawanyiko wao, wakati ambao hali hii haitafutii ufumbuzi wimbi la wahamiaji wanaondelea kuingia barani Ulaya, wakipitia Uturuki.

Rais wa Ufaransa François Hollande , kwa upande wake, ametaka suala hili" gumu la kugawana wahamiaji kwa idadi sawa " lipatiwe kabla ya mkutano huo.

Kugawana " wakimbizi ni moja ya sheria za hifadhi ", ambayo inapaswa kutekelezwa kati ya " nchi zote za Ulaya, hakuna nchi hata moja ambayo inaweza kupinga hali hii au hatuko tena katika umoja wetu ambao unasimamia kwa maadili na kanuni ", ameongeza rais Hollande.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kwa upande wake, amesisitiza mjini Berlin kwamba utatuzi wa mgogoro wa uhamiaji ulikua unategemea kwa kiasi kikubwa juu muendelezo au la wa vita nchini Syria, ambapo raia, " wameonekana wakikata tamaa kutokana na vita hivyo " na kuamua kukimbilia uhamishoni.

Marekani inatazamiwa kuwapokeawa mwaka ujao wakimbizi 85,000, ikiwa ni pamoja na raia 10,000 wa Syria, na 100,000 mwaka 2017, ametangaza John Kerry.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.