rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Serbia Ujerumani Hungary

Imechapishwa • Imehaririwa

Wahamiaji wanaozuiliwa Serbia watafuta barabara nyingine

media
Wahamiaji wa Septemba 15, 2015 katika mji wa Horgos nchini Serbia karibu na mpaka na Hungary. Photo par ELVIS BARUKCIC/AFP

Mamia ya wahamiaji wamekwama katika mpaka wa Serbia na Hungary huku wakilazimika kulala nje kwenye kibaridi kikali kutokana na mpaka wa hungary kufungwa.


Ripoti zinasema kuwa wahamiaji hao wengi wao kutoka nchini Syria wameanza kutafuta njia nyingine ya kwenda katika mataifa mengine ya Ulaya.

Hungary imeweka uzio kuwazuia wahamiaji hao lakini pia kupitisha sheria za kuwazuia wahamiaji kuingia katika ardhi yao.

Zoltan Kovac, msemaji wa serikali hiyo amesema wahamiaji ambao wanaweza kuruhusiwa ni wale waliokubaliwa rasmi kuingia nchini humo kupewa hifadhi ya kisiasa.

Austria pia imetangaza kudhibiti mipaka yake kuwazuia wahamiaji hao kuingia wengi wao wakiwa na lengo la kufika Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameitisha mkutano wa dharura kuzungumzia wimbi hili la wahamiaji.