Pata taarifa kuu
UJERUMANI-AUSTRIA-EU-WAKIMBIZI-USALAMA

Ujerumani yapokea idadi kubwa ya wahamiaji, Vienna yatoa wito kwa EU

Jumapili mwishoni mwa juma hili, Ujerumani imekua ikikaribisha idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Hungary wakipitia Austria, kwa nyimbo, chakula na mavazi. Hata hivyo, Vienna imetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kutafuta haraka jawabu la pamoja katika suala hilo.

Mkimbizi akiaungusha kilio alipowasili katika kituo kikuu cha treni cha Dortmund, Ujerumani magharibi, Septemba 6, 2015.
Mkimbizi akiaungusha kilio alipowasili katika kituo kikuu cha treni cha Dortmund, Ujerumani magharibi, Septemba 6, 2015. MAJA HITIJ/DPA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na uzito wa mgogoro huo uliochochewa na migogoro katika Mashariki ya Kati, Papa Francis amezitolea wito Jumapili Septemba parokia zote za Kikatoliki barani Ulaya kila moja kupokea familia moja ya wakimbizi.

Polisi ya Ujerumani imetoa idadi kubwa ya wakimbizi wapya 10,000 waliowasili nchini humo wakitokea Austria kwa siku ya Jumapili mchana pekee, baada ya kuorodhesha wakimbizi wengine 7,000 siku moja kabla, ambao wamekua wakipokelewa kila mahali na majeshi ya kujitolea kwa mabango yalioandikwa "Karibu Ujerumani".

" Watu wanatuhudumia vizuri hapa, wanatuhudumia kama binadamu, si kama nchini Syria ", amesema Muhammad, mkimbizi mwenye umri wa miaka 32 kutoka mji wa Syria wa al-Qusayr unaoendelea kukumbwa na machafuko.

Katika mji wa Frankfurt, usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, umati wa watu wakiimba " Huu ni mshikamano wa kimataifa ", huku kukiwa na makofi na kushangilia, wamekua wakiwapokea watu ikiwa ni pamoja na wanaume, wanawake na watoto, ambao wameonekana wamechoka na safari yao ndefu.

Wakati ambapo Ulaya ikigawanyika, kwa sasa inakabiliwa na migogoro mibaya zaidi ya wahamiaji tangu mwisho wa Vita vikuu vya II vya dunia, Berlin kwa upande wake imelegeza sheria zake kwa kuwapokea raia kutoka Syria, huku ikipinga uamzi wa kuwarejesha katika eneo lao walikoingilia barani Ulaya.

Katika uamuzi usiyokuwa wa kawaida, Austria ilikubali usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, kwa ushirikiano pamoja na Berlin, kuwarahisishia maelfu ya wakimbizi waliozuiliwa nchni Hungary kwa mapokezi na sehemu za kupitia ili kuingia Ujerumani Hungary ilishuhudia wimbi la wakimbizi 50,000 walioingia nchini humo kwa mwezi wa Agosti pekee.

Uamuzi huu hata hivyo ni wa "muda", ameonya Jumapili, Kansela Werner Faymann, akibainisha kuwa "uamzi wa aina hii haiwezi kuwa suluhu ".

Katika mahojiano ya simu Jumamosi, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri mkuu wa Hungary, Viktor Orban, walikubaliana kwamba Hungary na Ujerumani wanatakiwa kutimiza wajibu wa Umoja wa Ulaya " na kwamba wimbi hili la wakimbizi lililoshuhudiwa mwishoni mwa wiki hii limekua la kipekee", amesema Kansela Angela Merkel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.