Pata taarifa kuu
UGIRIKI-IMF-EU

Ugiriki yaomba mkopo mwingine toka umoja wa Ulaya wakati huu ikishindwa kulipa deni lake kwa IMF

Nchi ya Ugiriki imeanzisha harakati nyingine kwenye umoja wa Ulaya kwa kuwasilisha mapendekezo mengine mapya ya kuomba mkopo kutoka kwa nchi wanachama, wakati huu taifa hilo likishindwa rasmi kulipa deni lake kwa shirika la fedha duniani IMF. 

Ugiriki inataka mkopo mwingine kutoka umoja wa Ulaya
Ugiriki inataka mkopo mwingine kutoka umoja wa Ulaya Reuters
Matangazo ya kibiashara

Harakati hizi mpya za Ugiriki zimeanza wakati huu ambapo mawaziri wa fedha wa umoja huo, wanaketi hii leo kupitia mapendekezo mapya ya Uguriki ambayo inaonekana kulegeza msimamo na kukubali kuwa na mazungumzo mapya na wakiopeshaji wake.

Jumanne ya wiki hii nchi hiyo ilitakiwa iwe imelipa deni lake kwa IMF kutokana na makubaliano ya awali ambapo ndio ulikuwa muda wa mwisho mwa nchi hiyo kulipa deni lake, lakini ikashindwa kufanya hivyo kwa wakati.

Nchi ya Ugiriki inayokabiliwa na hali mbaya kiuchumi na kifedha, inakuwa taifa la kwanza lililoendelea kushindwa kulipa deni lake kwa wakati kwa shirika la fedha duniani IMF, deni ambalo lilikuwa la kiasi cha Euro bilioni 1.5.

Kwa sasa nchi ya Ugiriki inajaribu kuwashawishi viongozi wa Ulaya kulegeza masharti yao, ili kuiwezesha kupata fedha kwa wakati kujiendesha, pamoja na kuhakikisha kuwa haiondoki kwenye jumuiya ya Ulaya.

Mazungumzo kati ya viongozi wa Athens na wale wa Ulaya yameanza tena hii leo ambapo nchi hiyo iliwasilisha mapendekezo mapya ya muda wa miaka mwili kwa nchi hiyo kuwa na uwezo wa kupewa mkopo mwingine wa ziada.

Utawala wa Athens unaomba kiasi cha Euro bilioni 29.1 kutoka kwenye mpango wa dharura wa Umoja wa Ulaya.

Maafisa wa Ugiriki wameonesha kuwa tayari kuahirisha kura ya maoni waliyopanga ifanyike Jumapili hii iwapo viongozi wa Ulaya watakuwa tayari kukubaliana na maombi yao mapya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.