Pata taarifa kuu
UFARANSA-SAUDI ARABIA-QATAR-DIPLOMASIA

Riyadh: Hollande aalikwa katika mkutano wa nchi za Ghuba

Baada ya ziara ya saa chache nchini Qatar, rais wa Ufaransa François Hollande, amewasili tangu Jumatatu jioni wiki hii katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh ili kukutana kwa mazungumzo na Mfalme Salman.

François Hollande akiwasili Riadh, Jumatatu Mei 4 mwaka 2015, akipokelewa na Mfalme wa Saudi Arabia Salman.
François Hollande akiwasili Riadh, Jumatatu Mei 4 mwaka 2015, akipokelewa na Mfalme wa Saudi Arabia Salman. REUTERS/Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo nchini Saudi Arabia, Hollande anatazamiwa leo Jumanne kushiriki katika mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano la nchi za Ghuba. Baraza hilo linaundwa na Saudi Arabia, Qatar, Falme za Kiarabu, Koweit, Bahrein na Oman. Ni kwa mara ya kwanza rais kutoka nchi za magharibi kushiriki katika mkutano wa Wafalme kutoka nchi za Ghuba.

" Ni heshima ", amesema François Hollande jana Jumatatu akielezea mwaliko huo aliyopewa. Wengi wamekua wakijiuliza kwa nini Ufaransa imeonekana kuwa ni nchi muhimu na kualikwa katika mkutano huo wa Wafalme wa nchi za Ghuba?

" Tunafanya kazi ili kupata ufumbuzi wa kisiasa kuunga mkono shughuli wakati zinapohitajika, katika nyanja ya kijeshi. Tutahakikisha kuwa Syria inakua na serikali ya mpito, ambapo Bashar Al Assad hatashirikishwa katika serikali hiyo. Kila mmoja anaelewa hilo. Tupo pia katika muungano nchini Iraq kuchukua hatua dhidi ya ugaidi. Tunatoa mchango wetu pia katika diplomasia kufikia makubaliano na Iran juu ya mpango wake wa nyuklia, na unajua ni kiasi gani tuko umakini ili makubaliano hayo yawe kweli hakikisho kwamba Iran haiendelei na mpango wake wa nyuklia ", amejibu rais Hollande.

Hii ni ziara ya nne ya Hollande nchini Saudi Arabia. Ufaransa imepongeza kazi kubwa iliyofanya miaka ya hivi karibuni kwa kufufua uhusiano na Saudi Arabia. uhusiano huo uliingia matatani wakati wa utawala wa miaka mitano ya Nicolas Sarkozy.

Ufaransa inaonyesha kuwa imara katika masuala ya kikanda: katika majadiliano na Iran, kusaidia operesheni nchini Yemen na kuendelea kudai kuondoka kwa Bashar Al-Assad nchini Syria. Ufaransa inachukuliwa kama " rafiki muaminifu wa karibu " katika Ghuba, kulingana na kauli aliyotumia François Hollande Jumatatu wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.