Pata taarifa kuu
EU-Uchaguzi

Juncker kutawazwa raisi Mpya wa tume ya bara Ulaya

Viongozi wa muungano wa ulaya wanaokutana katika jiji la Brussels nchini Ubelgiji wanatarajiwa kumtawaza aliyekuwa waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Junker kuwa rais mpya wa tume ya bara Ulaya licha ya upinzani mkali kutoka Uingereza.

Jean-Claude Juncker anataraji kutawazwa kuongoza tume ya Umoja wa Ulaya
Jean-Claude Juncker anataraji kutawazwa kuongoza tume ya Umoja wa Ulaya REUTERS/Ints Kalnins
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kuwa haoni uwezekano wake kushinda katika tukio hili, dhidi ya Junker,lakini amesisitiza kuwa atafuata kanuni zake yeye mwenyewe.

Anaamini kuwa Junker anapendelea umoja wa kisiasa na hili laweza kudhuru mabadiliko katika umoja huo wa Uropa.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye alilaumu London kwa kumpinga Junker alimsifu kwa uzoefu wake na kusema kuwa junker atakuwa msikivu kwa kutekeleza matakwa ya nchi wanachama na bunge la Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.