Pata taarifa kuu
SPAIN

Wananchi wa Uhispania waandamana kushinikiza kupigwa kura ya maoni kuamua kuwa na utawala wa kifalme au la

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Uhispania wamewekwa kwenye hali ya tahadhari wakati huu maelfu ya raia kwenye miji ya Madrid na Barcelona wakiandamana kushinikiza bunge la nchi hiyo kupitisha sheria kufuta utawala wa kifalme kwenye taifa hilo. 

Mfalme wa Hispania, Juan Carlos akiwa na mwanae Felipe anayetarajiwa kurithi nafasi ya baba yake
Mfalme wa Hispania, Juan Carlos akiwa na mwanae Felipe anayetarajiwa kurithi nafasi ya baba yake Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya yanafanyika ikiwa imepita siku moja tu, toka mfalme Juan Carlos aliyeoongoza taifa hilo kwenye mabadiliko ya Kidemokrasia na kiuchumi kutangaza nia yake ya kumuachia mtoto wake Felipe.

Mfalme wa Hispania, Juan Carlos ambaye ametangaza nia ya kuachia nafasi yake
Mfalme wa Hispania, Juan Carlos ambaye ametangaza nia ya kuachia nafasi yake ©Reuters.

Wananchi wanataka kuitishwa kwa kura ya maoni kuamua iwapo wanaunga mkono kuendelea kuwepo kwa utawala wa kifalme kwenye taifa hilo au la,kwa kile baadhi yao wanachodai utawala huo umekuwa ukiongeza gharama za matumizi ya Serikali.

Kuanzia hii leo bunge la nchi hiyo litaketi kutunga sheria maalumu itakayoruhusu mchakato wa kufanyika mabadiliko ya kiutawala kuanza, mabadiliko ambayo sasa yatashuhudia mwana mfalme Felipe wa Sita akirithi kiti hicho.

Saa chache baada ya mfalme Carlos kutangaza kumaliza utawala wake wa zaidi ya miaka 39 toka kwenye utawala wa kiimla na kuingia kwenye demokrasia, tayari Serikali imeanza mchakato wa kitendo hiki kufanyika.

Wananchi wa Uhispania kwenye mji wa Madrid wakiandamana
Wananchi wa Uhispania kwenye mji wa Madrid wakiandamana REUTERS/Paul Hanna

Waziri mkuu Mariano Rajoy hapo jana mchana aliitisha mkutano wa dharura wa baraza lake la mawaziri kujadili na kisha kutunga sheria ambayo itaruhusu mabadiliko haya ya kiungozi kufanyika.

Mfalme Carlos anatajwa kuwa miongoni mwa watawala wa kifalme ambao ni maarufu zaidi duniani licha ya kashfa ya rushwa iliyowahi kumkumba mwaka 2012 ambapo alifanya ziara kwenye nchi ya Botswana kuwinda tembo, ziara ambayo inadaiwa alitumia fedha za walipakodi wa Uhispania.

Licha ya siku za hivi karibuni utawala wa kifalme nchini humo kupoteza umaarufu na iamni yake kwa wananchi, bado mfalme Carlos anakumbukwa kwa utawala wake makini uliopelekea mabadiliko ya demokrasia na kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.