Pata taarifa kuu
Thailand

Jeshi la Thailand huenda likamshikilia Shinawatra na viongozi wenzake kwa juma moja

Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand Yingluck Shinawatra pamoja na viongozi wengine wa kisiasa wanaoshikiliwa na jeshi nchini humo baada ya mapinduzi,huenda wakashikiliwa kwa hadi juma moja jeshi hilo limesema leo Jumamosi.

Mkuu wa majeshi ya Thailand jenerali Prayuth Chan-ocha
Mkuu wa majeshi ya Thailand jenerali Prayuth Chan-ocha REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa mara ya kwanza na vyombo vya habari msemaji wa jeshi hilo kanali Winthai Suvaree amesema kuwa huenda viongozi hao wakashikiliwa kwa juma moja kutegemeana na namna walivyohusika kuchochea mgogoro nchini humo.

Hatima ya Yingluck na viongozi wengine katika serikali iliyoondolewa madarakani na jeshi pamoja na chama chake haijulikani tangu walipoitwa na jeshi mapema jana Ijumaa.

Mkuu wa majeshi nchini humo ambaye pia amejitangaza kuwa waziri mkuu Prayuth Chan Ocha aliwaandikia barua viongozi wa serikali iliyoondolewa madarakani na kuwapiga marufuku kusafiri nje ya nchi hiyo.

Siku ya Alhamisi Jeshi nchi humo lilitangaza kuchukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo na kutangaza hali ya hatari na kutotembea nyakati za usiku, baada ya mahakama nchini humo kumwondoa madarakani aliye kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Yingluck Shinawatra.

Hata hivyo hatua ya jeshi hilo imekosolewa na dunia nzima huku Marekani ambayo imesisitiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia imechukua hatua ya kusitisha msaada wa dola milioni 3.5 kwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.