Pata taarifa kuu
Uingereza-Ireland

Ziara ya Malkia Elizabeth nchini Ireland yaandamwa na vitisho vya mashambulizi

Siku moja kabla ya malkia Elizabeth ii wa Uingereza kuzuru nchini Ireland,polisi nchini Uingereza imesema imepokea tishio la bomu kutoka kwa kundi moja la kigaidi lenye maskani yake nchini Ireland.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka makao makuu ya pilisi ya Uingereza zinaeleza kuwa tishio hilo halijaainisha sehemu wala muda utakaotekelezwa tukio hilo.

Kufuatia tishio hilo polisi walifunga barabara inayoelekea kasri ya Buckingham kwa saa kadhaa lakini hawakufanikiwa kupata kitu chochote kilichotiliwa shaka.

Ziara ya siku nne ya malkia Elizabeth ii inaratibiwa kwa uangalifu mkubwa kutokana na vitisho kutoka kwa makundi ya waasi wa Ireland ambao wanapinga viongozi wa Uingereza kukanyaga katika ardhi ya nchi hiyo.
 

Polisi wameimarisha ulinzi katika mipaka ya nchi hizo na tayari imewatia nguvuni waasi kadhaa ambao walihofiwa wataharibu ziara hiyo ya kihistoria ya Malikia Elizabeth ii.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.