Pata taarifa kuu
SENEGAL-WATOTO WA MITAANI

Senegal yakabilaina na watoto wa mitaani

Watoto wa mitaani wamefikia idadi ya 80,000 nchini Senegal kwa mujibu wa mashirika yasio ya kiserikali, huku mashirika mengine yakibaini kwamba ni zaidi ya idadi hiyo. Wengi wa watoto hao wamekua wakizurura hovyo mitaani.

Watoto wa mitaani wakikusanyika katika kituo cha mapokezi cha Ginddi, Dakar.
Watoto wa mitaani wakikusanyika katika kituo cha mapokezi cha Ginddi, Dakar. RFI/Guillaume Thibault
Matangazo ya kibiashara

Baada ya matangazo, Serikali iliamua Alhamisi Juni 30 kukabiliana na tatizo hili kwa kuwapeleka watoto zaidi ya 150 katika vituo vya mapokezi na kutangaza vikwazo.

Kikosi kinachojihusisha na masuala ya watoto kiliendesha Alhamisi hii operesheni ya kukamata watoto mitaani wakiomba omba. Operesheni hii inaongozwa na Niokhobaye Diouf, mkurugenzi wa haki na ulinzi kwa watoto. "Tunaendesha operesheni za usalama kwa watoto hawa. Wako katika hatari kutokana na mazingira yanayowazunguka, " Bw Diou amesema.

Watoto, waliochakarika, wakivaa nguo chafu, kubwa au zilizochanika walipelekwa katika kituo cha mapokezi cha Ginddi, katika mji wa Wolof. Hatua ya kwanza: kuwatambua. "Baada ya zoezi hili, itakuwa ni muda wa kuwauliza maswali kuhusu kwa nini wako hapa, Senegal. "

Suala hili la watoto wa mitaani limekua sugu katika nchi nyingi barani Afrika. Lakini nchi ambazo ziliondoka katika vita ndio zinashuhudia kwa kiasi kikubwa hali hii.

Wiki katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, polisi iliendesha operesheni ya kuwakamata watu kutoka tabaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wa mitaani, vijana wasiokuwa na ajira na wanawake (vijana kwa wazee wanaojihusisha na tabia ya omba omba) na kuwapeleka mikoani.

Hata hivyo mashirika yanayotetea haki za watoto yalilaani operesheni hiyo, yakibaini kwamba haki za watoto zinavunjwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.