Pata taarifa kuu

Houthi yaapa kulipiza kisasa baada ya kushambuliwa na Marekani na Uingereza

Nairobi – Waasi wa Houthi nchini Yemen, wameapa kulipiza kisasi baada ya Marekani na Uingereza kuwashambulia katika ngome zao, kwa kuyumbisha usalama kwenye Bahari ya Shamu.

Newly recruited fighters who joined a Houthi military force intended to be sent to fight in support of the Palestinians in the Gaza Strip, march during a parade in Sanaa, Yemen December 2, 2023. REUTE
Uongozi wa waasi hao, umetaja kushambuliwa kwa wapiganaji wake kama kitendo cha kihalifu REUTERS - KHALED ABDULLAH
Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa waasi hao, umetaja kushambuliwa kwa wapiganaji wake kama kitendo cha kihalifu na kuapa kuendelea kulenga meli zinazopitia kwenye Bahari hiyo kwenda nchini Israeli.

Iran nayo imeapa kuendelea kuwaunga mkono waasi hao ambao pia wanawaunga mkono wapiganaji wa kundi la Hamas kwenye mamlaka ya Palestina.

Mashambulio yaliyotekelezwa na ndege za kivita za Marekani na Uingereza, zililenga ngome 16 za waasi wa Houthi, ikiwemo ngome yake kuu na kuharibu silaha zake.

Waasi hao wamekuwa wakituhumiwa kwa kuteka meli katika bahari nyekundu
Waasi hao wamekuwa wakituhumiwa kwa kuteka meli katika bahari nyekundu via REUTERS - HOUTHI MILITARY MEDIA

Rais Joe Biden amesema kitendo hicho kitasaidia, kulinda meli zinazotumia Bahari hiyo ili kuendeleza biashara za Kimataifa, huku Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akisema, ilikuwa muhimu kutekeleza mashambulio hayo kwa ajili ya kujilinda.

Hata hivyo, Urusi imelaani mashambulio hayo, inayosema imekwenda kinyume cha sheria za Kimataifa, na kuishtumu Marekani na Uingereza kwa kutumia vibaya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililotaka waasi wa Houthi kuacha kushambulia meli kwenye Bahari ya Shamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.