Pata taarifa kuu

US:Raia 20 wauwawa katika shambulio la risasi mjini Lewiston,Maine

Nairobi – Takriban watu 20 wameuawa na makumi wengine wamejeruhiwa baada ya shambulio la risasi katika jimbo la kaskazini mwa Marekani la Maine. 

Shambulio la risasi laua raia zaidi ya 20 nchini Marekani
Shambulio la risasi laua raia zaidi ya 20 nchini Marekani AP - Rogelio V. Solis
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ni kuwa shambulio hilo la jana jioni lilitekelezwa katika uwanja wa mpira wa miguu na kwenye mkahawa.

Polisi wa eneo hilo walichapisha picha ya mpiga risasi huyo kwenye mtandao wa Facebook akiwa amebeba silaha inayoonekana kuwa ya nusu-otomatiki ndani ya eneo la tukio hilo.Na kufikia sasa ni kwamba mshukiwa hajakamtwa.

Vile vilepolisi imetoa wito kwa wafanyibiashara wa eneo hilo kusalia ndani hadi pale mshukiwa atakapopatikana.

Gavana wa  jimbo la Maine Janet Mills alisema "anafahamu na amefahamishwa kuhusu hali ya washambuliaji wa Lewiston."

Rais Joe Biden pia amefahamishwa, kulingana na Ikulu ya White House. Mbunge wa Maine Jared Golden aliandika kwenye mtandao wa  X, mbayo zamani ilijulikana kama Twitter kwamba amesikitishwa na kitendo hicho.

Marekani imerekodi  visa vya zaidi ya watu 500 waliouawa kwa kupigwa risasi mwaka huu.

Juhudi za kuimarisha udhibiti wa umiliki wa bunduki kwa miaka mingi zimeendelea dhidi ya upinzani kutoka kwa Republican, na kuwakandamiza watetezi wa haki ya kikatiba ya kubeba silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.