Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda akamatwa Uholanzi

Pierre-Claver Karangwa, ambaye ni afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda anayeshukiwa kuwa na jukumu muhimu katika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 amekamatwa nchini Uholanzi siku ya Jumanne, kulingana na waendesha mashtaka wa Uholanzi.

Ofisi za taasisi ya haki ya Ulaya, Eurojust, huko  Hague mnamo 2011.
Ofisi za taasisi ya haki ya Ulaya, Eurojust, huko Hague mnamo 2011. © Wikimedia Commons BY SA 3.0 Vincent van Zeijst
Matangazo ya kibiashara

Rwanda inamtuhumu Karangwa kwa kuhusika na mauaji ya Watutsi karibu 30,000 katika parokia ya Mugina karibu na mji mkuu wa Rwanda, Kigali mwezi Aprili 1994 na iliomba apelekwe nchini humo mwaka 2012.

Waendesha mashtaka nchini Uholanzi wamesema wanamshuku Karangwa kwa kuhusika katika kuchoma nyumba na wanawake na watoto kadhaa waliokuwemo ndani yake kufuatia shambulio hilo katika parokia ya Mugina.

Takriban watu 800,000 wa kabila la Watutsi na Wahutu wenye msimammo wa wastani waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, yaliyoongozwa na serikali ya Wahutu wenye itikadi kali.

Karangwa, ambaye ameishi Uholanzi tangu 1998, alikuwa na uraia wa Uholanzi uliofutwa juu ya mashtaka ya mauaji ya kimbari dhidi yake.

Katika kesi mahakamani kuhusu uwezekano wa kusafirishwa kwake Desemba 2022, Karangwa alisema hakuwa na hatia ya uhalifu aliotuhumiwa.

Hata hivyo Mahakama Kuu ilikanusha madai hayo kwa sababu Karangwa alikuwa mwanasiasa wa upinzani.

Karangwa, ambaye ameishi Uholanzi tangu 1998, alikuwa na uraia wa Uholanzi uliofutwa juu ya mashtaka ya mauaji ya kimbari.

Pierre-Claver Karangwa, mwenye umri wa miaka 67, alikamatwa katika uchunguzi wa Uholanzi kuhusu jukumu lake katika mauaji ya kimbari, ambayo waendesha mashtaka waliuanza baada ya Mahakama Kuu ya Uholanzi mwezi Juni mwaka huu kusema kuwa hawezi kupelekwa nchini Rwanda kwa hofu ya kwamba kesi yake isingekuwa ya haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.