Mshirika wa zamani wa Prigozhin kuongoza wapiganaji wa kujitolea Ukraine
Nairobi – Andrei Troshev, kamanda za zamani wa mamluki wa Wagner, amepewa jukumu la kuvisimamia vikosi vya wapiganaji wakujitolea nchini Ukraine, baada yake kukutana na rais Vladimir Putin ambaye alimpa majukumu hayo.
Imechapishwa:
Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov , kiongozi huyo wa zamani wa Wagner kwa sasa ni mfanyikazi wa wizara ya ulinzi ya Urusi.
Uteuzi wake katika wadhifa huo umeafikiwa baada ya kikao kati yake ya rais Vladimir Putin, kilichojadili nafasi ya wapiganaji wa kujitolea katika mzozo wa Ukraine.
Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanasema hatua hii ya kremlin huenda inatuma ujumbe kwa dunia kuwa Urusi kwa sasa imechukua uthibiti wa Wagner baada ya jaribio la uasi dhidi ya utawala wa Putin mwezi Juni kutofanikiwa.
Msikilizaji ikumbukwe kuwa uasi huo wa muda mfupi uliongozwa na mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin, ambaye baadae mwezi Agosti alidaiwa kufariki katika ajali ya ndege.
Troshev alihusika pakubwa katika oparesheni za Wagner wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria kwa mujibu wa stakabadhi za Umoja wa Ulaya.