Pata taarifa kuu

Ukraine yadai kufanya shambulio la ndege zisizo na rubani nchini Urusi, ikiwa ni mara ya kwanza

Ukraine imedai kutumia ndege zisizo na rubani zilizorushwa kutoka eneo la Urusi kushambulia uwanja wa ndege wa kijeshi wa Pskov usiku wa Jumanne Agosti 29 kuamkia Jumatano Agosti 30, mkuu wa kijasusi wa kijeshi wa Ukraine alitangaza siku ya Ijumaa jioni Septemba 1. Jiji la Pskov linapatikana kilomita 700 kutoka mpaka na Ukraine.

Moshi ukifumba karibu na mji wa Urusi wa Pskov mnamo Agosti 29, 2023, huku urusi ikiishutumu Ukraine kwa kutekeleza idadi kubwa ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya malengo tofauti ya Urusi.
Moshi ukifumba karibu na mji wa Urusi wa Pskov mnamo Agosti 29, 2023, huku urusi ikiishutumu Ukraine kwa kutekeleza idadi kubwa ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya malengo tofauti ya Urusi. AP - Ostorozhno Novosti
Matangazo ya kibiashara

Je, Ukraine inawezaje kushambulia malengo sahihi kama hayo kilomita mia kadhaa kutoka kwenye mipaka yake? Swali hilo limeibuka tangu shambulio la kushangaza lililofanywa mwanzoni mwa juma katika mkoa wa Pskov.

Akihojiwa na jarida maalumu la The War Zone, mkuu wa ujasusi wa kijeshi wa Ukraine Kyrylo Boudanov anatoa jibu: ndege zisizo na rubani hazikurushwa kutoka Ukraine, lakini kutoka eneo la Urusi. "Ndege zisizo na rubani zilizotumiwa kushambulia kambi ya anga ya Kresty huko Pskov zilirushwa kutoka ndani ya Urusi," amebaini.

Afisa huyo wa Ukraine alikataa kutaja ikiwa shambulio hilo lilifanywa na vijana wake au na Warusi wanaofanya kazi kwa niaba ya Kyiv. Lakini jarida hilo, kwa kuzingatia picha iliyopigwa na moja ya ndege zisizo na rubani, linakadiria kuwa waliofanya shambulio hilo walikuwa karibu na kambi ya kijeshi.

Kwa mujibu wa The War Zone, ndege zisizo na rubani zilizotumika hazikuwa ndege zisizo na rubani za kamikaze, lakini ndege zenye uwezo wa kurusha mabomu madogo.

Kwa mara ya kwanza Kyiv yakiri kutekeleza mashambulizu katika ardhi ya Urusi

Lengo ni kwenda mbali zaidi,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitangaza siku ya Alhamisi, Agosti 31.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kiev kukiri kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Urusi, ambako sio tu mashambulizi mengi ya ndege zisizo na rubani lakini pia vitendo vinavyodaiwa kuwa vya hujuma vimetokea, pamoja na uvamizi wa kutumia silaha. "Tunafanya kazi kutoka eneo la Urusi," Bw. Boudanov ameliambia jarida la The War Zone. Kremlin, kwa upande wake, ilikataa kutoa maoni juu ya dai hili.

Kyiv inajaribu kuleta uhasama nchini Urusi katikati ya mashambulio ya kukomboa maeneo yaliyokaliwa. Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yanayohusishwa na Ukraine na kulenga mji wa Moscow na miji mingine ya Urusi yamekuwa yakitekelezwa kila siku kwa miezi kadhaa, huku vikosi vya Urusi vikiendelea na mashambulizi yao makubwa katika miji ya Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.