Pata taarifa kuu

Vladimir Putin: Nasikitishwa na kifo cha Prigozhin lakini alifanya 'makosa'

Chini ya saa 24 baada ya kutangazwa kwa ajali ya ndege ya kibinafsi ambayo Yevgeny Prigozhin alikuwemo, na wakati ukimya wa mamlaka umeshuhudiwa nchini Urusi, Vladimir Putin amevunja ukimya huo siku ya Alhamisi joni na kuelezea kuhuzunishwa kwake na kifo cha "mtu aliyefanya makosa". Rais wa Urusi ametoa salamu za rambirambi kwa ndugu wa wahanga wa ajali hiyo.

Yevgeny Prigozhin  (kushoto) na Vladimir Putin (kulia), Septemba 20, 2010 huko St. Petersburg.
Yevgeny Prigozhin (kushoto) na Vladimir Putin (kulia), Septemba 20, 2010 huko St. Petersburg. AP - Alexei Druzhinin
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Moscow,

Rais wa Urusi Vladimir Putin amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu ajali ya ndege iliyotokea jana.

Ametuma salamu za rambirambi zake kwa familia za waliopoteza maisha, na anaelezea mwanzilishi wa Wagner Group Yevgeny Prigozhin kama mfanyabiashara mwenye talanta.

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni Putin, anasema wachunguzi wataangalia kilichotokea, lakini hilo litachukua muda

Rais wa Urusi amesema alifahamu Alhamisi asubuhi kuhusu ajali hiyo ya ndege.

Hawa ni watu ambao wametoa mchango mkubwa kwa lengo letu la pamoja la kupigana dhidi ya utawala wa Nazi mamboleo nchini Ukraine. Hatutasahau.

Aliyeripotiwa kuwa pamoja na Prigozhin kwenye ndege hiyo ni mtu wake wa mkono wa kulia Dmitry Utkin, pamoja na washiriki wengine watano wa Wagner na wafanyakazi watatu.

"Alifanya makosa makubwa maishani mwake. Alipata matokeo aliyohitaji, kwa ajili yake mwenyewe na kwa lengo la pamoja, kama miezi michache iliyopita. Rais wa Urusi haongei juu ya tuzo yake ya juu ya kijeshi kama "shujaa wa Urusi". Na kama anasema anamchukulia kama "mwenye kipaji", ni kama "mfanyabiashara ambaye alifanya kazi hasa barani Afrika", amesema rais wa Urusi.

Hatimaye, Vladimir Putin ameahidi: uchunguzi wa ajali hiyo iliyogharimu maisha ya watu kumi, ikiwa ni pamoja na Prigozhin na Dmitry Utkin, namba mbili wa Wagner, "utafanyika hadi mwisho".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.