Pata taarifa kuu

Urusi inasema imezuia mashambulio kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine

Urusi inasema, imezuia mashambulio kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine waliolenga viiji kadhaa katika jimbo la Donetsk, katika eneo ambalo limekuwa likishuhudia mapigano makali. 

Wanajeshi wa Ukraine kwa upande wao wamedai kuchukua baadhi ya vijiji vilivyokuwa vinakaliwa na Urusi
Wanajeshi wa Ukraine kwa upande wao wamedai kuchukua baadhi ya vijiji vilivyokuwa vinakaliwa na Urusi © 35th Separate Brigade of Marines via Facebook/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii ya Urusi inakinzana na ile ya Ukraine ambayo, ilisema wanajeshi wake walikuwa wamewashinda wale wa Urusi katika vijiji vinne ambavyo kwa sasa viko mikononi mwao. 

Wizara ya Ulinzi ya Urusi inasema  vikosi vyake vimewaondoa wanajeshi wa Ukraine karibu na mji wa Velyka Novosilka, ambao Kiev inasema inadhibiti. 

Mkanganyiko huu hata hivyo, unaelezwa na wachambuzi wa vita kuwa ni wazi kuwa Ukraine imeanza makabiliano yaliyokuwa yanasubiriwa, kuwaondoa wanajeshi wa Urusi katika ardhi yake, katika maeneo ya Mashariki. 

Katika siku za hivi karibuni, Ukraine imekuwa ikisema inaendelea kuchukua maeneo yake yaliyochukuliwa na Urusi, wakati huu rais Volodymyr Zelensky mwishoni mwa wiki iliyopita, akisema vikosi vyake vimeanza makabiliano ya kuikombo nchi yake. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.