Pata taarifa kuu

Raia nchini Uturuki wanajiandaa kupiga kura kesho.

Nairobi – Uchaguzi nchini Uturuki utafanyika kesho huku Upinzani ukiuangana dhidi yake  Rais wa sasa Recep Tayyip Erdogan aliyeingia madarakani mwaka 2014.Erdogan pia aliwahi kuwa waziri mkuu nchini humo kwa takribani miaka 11.

Picha za wagombea Urais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kushoto) na Kemal Kilicdaroglu (kulia).
Picha za wagombea Urais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kushoto) na Kemal Kilicdaroglu (kulia). © Ozan Kose / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uturuki na mwenye ushawishi mkubwa Recep Tayyip Erdogan yupo kwenye kinyang’anyiro kikali dhidi yake , Kemal Kilicdaroglu,ambaye ijumaa alifanya mkutano wake wa mwisho ili kushawishi raia nchini humo kumpigia kura.

Erdogan amesema kuwa kwa miaka 20 iliyopita amesaidia ,nchi hiyo pakubwa licha ya changamoto zote za kiuchumi ,mfumuko wa bei na hata majanga kama  tetemeko la ardhi  lilloshudiwa februali.

Vilevile mgombea  mwenza , Kemal  mwenye umri wa miaka 74 amesema kuwa nia yake kuu ni kurejesha amani na democrasia.Kemal Kilicdaroglu ni kiongozi wa chama cha Republican People's Party na ameibuka kuwa mpinzani mkuu wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika uchaguzi huo wa kihistoria. Kilicdaroglu amekuwa kiongozi wa Kambi Kuu ya Upinzani nchini tangu 2010.

Kufikia sasa Kilicdaroglu anaonekana kua mbele katika kura za maoni na wafuasi wake wameapa kuwa kiongozi huyo ataibuka mshindi kwa Zaidi ya asilimia 50% ya kura, badala ya kukabiliwa na duru ya pili wiki mbili baadaye.

Firat, mmoja wa wapiga kura milioni tano kwa mara ya kwanza, alisema alifurahishwa na wahafidhina na wazalendo wanaojitokeza kwenye jukwaa moja na mkuu wa chama cha mrengo wa kati cha Republican People's Party (CHP).

Rais Tayyip Erdogan alitangaza tarehe  ya uchaguzi baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuwaua zaidi ya watu 45,000 nchini Uturuki. "Taifa hili litafanya kile kinachohitajika Mei 14, Mungu akipenda," Erdogan alisema katika hotuba yake kwa wabunge kutoka chama chake tawala cha AK bungeni.

Kumekuwa na ishara zinazokinzana kuhusu uwezekano wa muda wa uchaguzi wa urais na ubunge tangu tetemeko la ardhi la miezei iliopita huku wengine wakieleza kuwa huenda uchaguzi ukaahirishwa hadi baadaye mwaka huu au usifanyike kama ilivyopangwa.

Kabla ya mkasa huo umaarufu wa Erdogan ulikuwa umeporomoka kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha na kushuka kwa sarafu ya Uturuki ya Lira. Tangu wakati huo amekuwa akikabiliwa na wimbi la ukosoaji kufuatia hatua ya serikali yake kukabiliana na tetemeko baya la ardhi kuwahi kutokea katika historia ya taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.