Pata taarifa kuu

Ajali ya boti ya wahamiaji Calabria: Upinzani Italia wapaza sauti kukabiliana na uhamiaji

Baada ya ajali mbaya ya boti katika pwani ya Crotone, huko Calabria, iliyogharimu maisha ya watu wasiopungua 59, ikiwa ni pamoja na watoto karibu ishirini, wakati waokoaji waliokoa maisha ya wahamiaji 80 na bado wanatafuta idadi ya watu waliokosekana, watu mbalimbali wameanza kupaza sauti na kuomba Umoja wa Ulaya kufanya kilio chini ya uwezo wao kukabiliana na suala hili la uhamiaji kupitia Bahari ya Mediterania pamoja na uwajibikaji na ubinadamu.

Idara husika ikipakia jeneza la mmoja wa wahamiaji waliokufa maji katika gari Jumapili hii, Februari 26, 2023 karibu na Steccato di Cutro Beach, kusini mwa Crotone nchini Italia, katika pwani ya  Calabria.
Idara husika ikipakia jeneza la mmoja wa wahamiaji waliokufa maji katika gari Jumapili hii, Februari 26, 2023 karibu na Steccato di Cutro Beach, kusini mwa Crotone nchini Italia, katika pwani ya Calabria. AFP - ALESSANDRO SERRANO
Matangazo ya kibiashara

Boti ya takriban mita ishirini ambayo ilisafirisha takriban "wahamiaji 250" kulingana na baadhi ya shuhuda, kutoka Uturuki, anaripoti mwandishi wetu huko Roma, Anne Le Nir. Kwa mujibu wa waokoaji waliokuwa kazini tangu asubuhi ya Jumapili hii, boti iliyojaa wahamiaji wenye asili ya Afghanistan, Iran na Pakistan ilizama, kutokana na dhoruba kali, dhidi ya miamba karibu na ufuo wa Steccato di Cutro.

Waziri Mkuu Giorgia Meloni ameelezea katika taarifa yake "maumivu makubwa kwa waathiriwa wa wasafirishaji haramu wa binadamu na akasisitiza dhamira ya serikali yake ya kuzuia uhamiaji haramu". Waziri wa Mambo ya Ndani, Matteo Piantedosi alimuunga mkono kwa kuzungumzia "janga kubwa linalodhihirisha kuwa ni muhimu kupambana na mitandao ya wahamiaji haramu".

Upinzani nchini Italia umeishushia lawama serikali ya Giorgia Meloni, huku ukiumba Umoja wa Ulaya kutafakari na kufanya kilio chini ya uwezo waio kukabilina na wimbi la wahamiaji wanaotafuta kuvuka bahari kuingia Ulaya, huku wakihuzunishwa na njia hatari wanazotumia wahamiaji kwa kuweza kufikia malengo yao.

Kwa upande wake, shirika lisilo la kiserikali la Sea Watch liliandika kwenye Twitter "kutokuwepo kwa ujumbe wa utafiti wa Ulaya ni uhalifu unaorudiwa kila siku". 

Shuhuda zilizokusanywa na vyombo vya habari vya Italia, hasa zile kutoka kwawaokoaji, ni za kuhuzunisha. Moja inasema kwamba ni wale tu ambao waliweza kuruka kutoka kwenye bot waliweza kunusurika, wale ambao walikuwa wamerundikana katika boti wote walifariki. Picha zinaonyesha miili iliyofunikwa kwenye begi nyeupe ya plastiki yenye nambari iliyoandikwa kwenye kila mfuko.

Ajali hiyo mpya ya boti inakuja siku chache tu baada ya bunge kupitisha sheria mpya zenye utata na serikali yenye siasa kali za mrengo wa kulia juu ya kuwaokoa wahamiaji. Mkuu wa serikali Giorgia Meloni, kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Fratelli d'Italia (FDI), alichukua wadhifa wa kiongozi mkuu wa muungano mwezi Oktoba baada ya kuahidi kupunguza idadi ya wahamiaji wanaowasili Italia.

Sheria hiyo mpya inazitaka meli za kibinadamu kufanya uokoaji mmoja tu kwa wakati mmoja, jambo ambalo wakosoaji wanasema linaongeza hatari ya vifo katika eneo la kati la Mediterania ambalo kivuko chake kinachukuliwa kuwa hatari zaidi duniani kwa wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.