Pata taarifa kuu

NATO: Sweden na Finland zinafa kukubaliwa kuwa wanachama.

NAIROBI – Katibu mkuu wa jumuiya ya NATO, Jens Stoltenberg, amesema wakati umefika kwa nchi za Sweden na Finland, kukubaliwa kuwa wanachama wapya wa jumuiya hiyo, wakati huu ukanda wa Ulaya ukikabiliwa na tishio la Urusi.

Jens Stoltenberg, Mkuu wa NATO
Jens Stoltenberg, Mkuu wa NATO AP - Olivier Matthys
Matangazo ya kibiashara

Akiwa mjini Ankara, ambako pia amejionea uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi, Jens amesema kwa usalama wa ukanda, ni lazima nchi hizo ziiingizwe haraka.

“Finland na Sweden wameongeza ushirikiano na Uturuki kukabiliana na ugaidi kwa hivyo ni muda wa kuikubali nchi hizo mbili kama wanachama wa NATO.”amesemaJens Stoltenberg

Mataifa ya Sweden na Finland yamekuwa yakitaka kwa muda sasa kupewa unachama wa NATO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.