Pata taarifa kuu

Shambulio kubwa la kombora lalenga Kyiv na maeneo mawili ya nishati karibu na Odessa

Mtu mmoja ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa huko Kyiv siku ya Alhamisi asubuhi baada ya  jeshi la Urui kudondosha makombora kadhaa katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv. Maeneo mawili muhimu ya nishati katika mkoa wa Odessa pia yaliharibiwa na mashamblizi ya makombora.

Wakazi wa Kyiv wamekimbilia katika treni ya mwendo kasi kufuatia mashambulizi mapya ya Urusi, Alhamisi hii, Januari 26, 2023.
Wakazi wa Kyiv wamekimbilia katika treni ya mwendo kasi kufuatia mashambulizi mapya ya Urusi, Alhamisi hii, Januari 26, 2023. AP - Efrem Lukatsky
Matangazo ya kibiashara

Shambulio la maombora limefanyika Alhamisi asubuhi dhidi ya Ukraine. "Ndege sita za kivita aina ya Tu-95 zilipaa kutoka eneo la Murmansk na kurusha makombora," Yuri Ignat, msemaji wa jeshi la anga la Ukraine, ameiambia televisheni.

Jengo lisilo la makazi lilipigwa katika wilaya ya Holosiivsky mjini Kyiv Alhamisi asubuhi, na kuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine wawili, Meya wa Kyiv Vitali Klitschko ameripoti. Kulingana na utawala wa kijeshi wa mji mkuu, kipande cha kombora kilianguka kwenye kitongoji na kumuua mzee wa miaka 55. Vitali Klitschko pia aesema kuwa milipuko kadhaa imetokea katika wilaya ya Dniprovsk, kwenye Ukingo wa kushoto wa mji wa Kyiv. "Mlipuko waripotiwa huko Kyiv! msalie kwenye makazi yenu, " Meya wa mji mkuu wa Ukraine, Vitali Klitschko, alisema mapema kwenye Telegram.

Mfumo wa ulinzi wa angani  ulmeharibu makombora 47 kati ya 55 yaliyorushwa na Urusi nchini Ukraine siku ya Alhamisi, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine Valery Zaluzhny ametangaza kwenye Telegram.

Kukatwa kwa umeme

Mikoa mingine imekumbwa na mashambulizi ya angani ya Urusi asubuhi. Makombora yalipigwa hasa katika mkoa wa Odessa. "Maeneo mawili muhimu ya miundombinu ya nishati katika mkoa wa Odessa yaliharibiwa," mkuu wa utawala wa kijeshi wa wilaya ya Odessa amesema katika taarifa. Mashambulizi haya hayakusababisha majeraha yoyote, amesema, huku akitoa wito kwa wakaazi wa jiji hilo kusalia katika makazi hayo.

Mashambulizi ambayo yamechelewesha kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna, akizuru mji wa bandari kuonyesha uungaji mkono wa Paris kwa Ukraine.

Kama athari za mashambulizi haya, kukatwa kwa umeme kwa "dharura" kulianzishwa Alhamisi asubuhi huko Kyiv na katika mikoa mitatu, limetangaza shirika la kibinafsi la umeme la DTEK. 

Wimbi hili jipya la mashambulizi ya Urusi linaonekana kuwa jibu la kijeshi la Moscow kwa tangazo la kutumwa kwa vifaru vizito na nchi washirika wa Ukraine. Msemaji wa Kremlin Dimitri Peskov amerejelea kwenye matangazo haya ya utoaji wa vifaru vizito. Na amesema, haya yanahusiana na "ushiriki wa moja kwa moja katika mzozo" wa nchi zinazounga mkono Kyiv. Mtazamo unaopingana kabisa na ule wa nchi washirika wa Ukraine ambao wanazungumza juu ya silaha za kujihami na zisizo za mashambulizi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amewasili Odessa, kusini-magharibi mwa Ukraine, siku ya Alhamisi kuonyesha uungaji mkono wa Paris wakati jiji hilo lilipopigwa na makombora mapya ya Urusi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.