Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Erdogan: Hatutaiunga mkono Sweden kujiunga NATO

Tangu mwezi Mei, Uturuki imeitaka Sweden kuwarejesha watu wanaotuhumiwa kwa ugaidi ili kuondoa kura yake ya turufu juu ya nchi hiyo kuingia katika Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO. Maendeleo yasiyotosheleza kwenye faili hiyo yanaudhi Ankara.

Katika picha hii iliyotolewa na ikulu ya rais wa Uturuki, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza baada ya kikao cha baraza la mawaziri mjini Ankara, Uturuki, Jumatatu, Januari 23, 2023.
Katika picha hii iliyotolewa na ikulu ya rais wa Uturuki, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza baada ya kikao cha baraza la mawaziri mjini Ankara, Uturuki, Jumatatu, Januari 23, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan hakutaka kuficha hasira yake Jumatatu, Januari 23, katika hotuba yake kwa taifa. Alitumia dakika tano za hotuba yake kukashifu tabia ya kutojali ya mamlaka ya Sweden wakati wa maandamano ya kupinga Uturuki ya siku za hivi karibuni.

Uidhinishaji uliotolewa kwa mwanaharakati wa chuki dhidi ya Uislamu kuchoma Quran mbele ya ubalozi wa Uturuki Jumamosi Januari 21 unakamilisha shambulio dhidi ya rais wa Uturuki, ambaye alizungumza kwa ukali:

Ni wazi kwamba wale walioidhinisha fedheha kama hiyo mbele ya ubalozi wa nchi yetu hawawezi tena kutarajia ishara kutoka kwetu kuhusu uanachama wao katika NATO. Mnahimiza mashirika ya kigaidi ambayo yanavuma kila mahali katika mitaa yetu, kisha mnaomba tuwaunge mkono kujiunga na NATO. Mnaishi dunia gani? Ikiwa mnawapenda, wateteeni na walindeni sana wanachama wa mashirika ya kigaidi na maadui wa Uislamu, basi tunawashauri muwakabidhi majukumu ya kuilinda nchi yenu.

Ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Sweden iliyopangwa kufanyika Alhamisi tarehe 27 tayariimefutwa na serikali. Kwa kauli hii ya mwisho, Sweden kujiunga kwenye Muungano wa Atlantiki ni kama mvua kunyesha katika msimu wa kipwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.