Pata taarifa kuu

Ujumbe wa Uturuki nchini Marekani kupata ndege za kivita za F-16

Kusitishwa kwa uwasilishaji wa ndege za kivita nchini Uturuki kutoka Marekani kumekuwa suala la mvutano kati ya nchi hizo mbili tangu mwaka 2019. Lakini faili inaendelea... Ujumbe wa Uturuki uko njiani kuzuru Washington Jumatatu Agosti 15.

Ndege ya kivita ya Uturuki F-16 ikipaa hewani katika kambi ya Incirlik, Julai 27 mwaka 2015.
Ndege ya kivita ya Uturuki F-16 ikipaa hewani katika kambi ya Incirlik, Julai 27 mwaka 2015. REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yanaonekana kuwa magumu kwa wajumbe wa Uturuki wanaosafiri kwenda Washington siku ya Jumatatu. Uturuki inaendelea kufanya kilio chini ya uwezo wake ili kupata ndege 40 za kivita za F-16 zilizoagizwa nchini Marekani.

Lakini tangu mwaka 2019, faili hii imeshindwa kupatiwa suluhu. Ankara imechagua kununua mfumo wa ulinzi wa ndege wa Urusi, maarufu S-400. Mpango ambao haukupendwa na Washington, ambayo ilisimamisha usafirishaji wa ndege za F-35 zilizoagizwa awali. Na tangu wakati huo, serikali ya Recep Tayyip Erdogan imezidisha mmvutano ili kuifanya Marekani ikubali.

Masharti yaliyoombwa na Congress

Rais Biden amejionyesha kuunga mkono kuwasilishwa kwa ndege hizo mwezi Juni, wakati wa mkutano wa NATO, lakini utambuzi wake utategemea uamuzi wa Bunge la Marekani. Maseneta kwa wanaitaka Uturuki kukubali kutotumia ndege katika anga ya Ugiriki.

Wizara ya Ulinzi ya Uturuki tayari imetangaza kuwa haiwezi kukubali sharti lililowekwa na maafisa wa Marekani waliochaguliwa. Kwa wakati huu, ni uingiliaji kati tu wa utawala wa Biden unaonekana kuwa na uwezo wa kubadilisha hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.