Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-SIASA

Mazungumzo ya njia ya simu kati ya Biden na Xi Jinping yasubiriwa

Rais wa Marekani Joe Biden hii leo anatarajiwa kufanya mazungumzo ya njia ya simu na mwenzake wa China Xi Jinping.

Joe Biden wa Marekani na  Xi Jinping wa China
Joe Biden wa Marekani na Xi Jinping wa China AFP - MANDEL NGAN,ANTHONY WALLACE
Matangazo ya kibiashara

Haya ni mazungumzo ya tano ya njia ya simu baina ya Viongozi hao wa wawili wanaongoza mataifa mawili yenye nguvu zaidi duniani, Biden na Xi Jiping wanatarajiwa kutumia muda huo kuangazia masuala kadhaa ya muhimu kati yao.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika wakati huu ambapo mvutano ukiwepo kati ya Washington na Beijing kutokana na mpango wa spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi kuataka kufanya ziara nchini Taiwan eneo ambalo China inadai ni mojawapo ya sehemu yake.

Taiwan tayari imeonya kuichukulia Washington hatua iwapo kiongozi huyo wa bunge ataendelea na ziara yake. Pelosi amekuwa akidai kuwa china inakiuka haki za binadamu na inafaa kushtumiwa.

Ofisi ya spika Pelosi bado haijathibitisha iwapo kiongozi huyo ataizuru Taiwan lakini mipango hiyo ya safari inatishia kuongeza mvutano baina ya mataifa hayo mawili ambayo tayari yanavutana kuhusu biashara na suala la haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.