Pata taarifa kuu
CANADA- MARIDHIANO

Ziara ya Papa Francis yenye matumaini nchini Canada

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis, yuko nchini Canada kwa ziara ya wiki moja, ambapo anatarajiwa kuziomba radhi jamii za wahanga wa vitendo vya udhalilishaji vilivyofanywa na makasisi wake katika shule zilizokuwa zinamilikiwa na kanisa hilo.

Papa Francis nchini Canada.
Papa Francis nchini Canada. REUTERS - GUGLIELMO MANGIAPANE
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kuanza ziara yake kuelekea Canada, Papa Francis, aliwaambia waandishi wahabari kuwa, ziara hii ni muhimu hasa ukizingatia masuala yaliyotokea.

Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Edmonton, Papa Francis alikaribishwa na waziri mkuu Justin Trudeau na kulakiwa na viongozi wa jamii za asili ambao walimpa maua na kushikana mikono.

Katika miaka kati ya 1980 na 1990, Serikali ya Canada iliwapeleka vijana zaidi ya laki 1 na elfu 50 kwenye vituo zaidi ya 139 vilivyokuwa chini ya Kanisa katoliki, ambapo walitenganishwa na wazazi wao, lugha na tamaduni.

Wengi wa walipelekwa kwenye vituo hivyo walifanyiwa udhalilishaji wa kingono na kutumikishwa kwa nguvu, huku maelfu wakidaiwa walifariki kutokana na utapiamlo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.