Pata taarifa kuu

Msaada wa kijeshi kutoka kwa mataifa ya magharibi ulifika kuchelewa: Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, ameelezea kughabishwa na hatua ya mataifa ya magharibi kuchelewa kutuma msaada wa kijeshi nchini humo kusaidia katika mzozo na urusi ambapo amesema maelfu ya raia hawengeuawa iwapo msaada huo ungetumwa mapema.

Dmytro Kuleba, waziri wa mambo ya kigeni ya Ukraine.
Dmytro Kuleba, waziri wa mambo ya kigeni ya Ukraine. AFP - FRANCOIS WALSCHAERTS
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu mkuu  wa intelejensia wa Marekani,  Avril Haines amewaambia wabunge kwamba rais Vladimir Putin anatazamia kufikia malengo yake ya kijeshi sio tu mashariki mwa Ukraine, baada yake kushindwa kuuteka mji wa Kyiv katika hatua za mwazo za vita vyake nchini Ukraine, Haines akisema hatua ya  vikosi vya urusi kuenda kwenye eneo la mashariki la Donbas ni ya muda tu.

Onyo hili la Marekani likija wakati ambapo mapigano makali yakiripotiwa kuenedelea mashariki mwa Ukraine eneo ambalo Urusi inajaribu kuchukua.

Ukraine yenyewe nayo inasema imechukua tena miji minne iliyokuwa imekaliwa na wanajeshi wa Urusi katika eneo la Kharkiv kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Miji ya Cherkasy Tyshky, Ruski Tyshky, Rubizhne Bayrak zote zikisemekana kurejeshwa tena mikononi wa Ukraine kutoka kwa Urusi kwa mujibu wa ripoti ya jeshi la taifa hilo.

Tayari Wabunge nchini Marekani, wameanza majadiliano kuhusu msaada wa dola za Marekani bilioni 40 kwa nchi ya Ukraine, bajeti ambayo inatarajiwa kupitishwa na wabunge kutoka vyama vyote.

Licha ya bajeti hii kupingwa na baadhi ya wabunge wa Republicans, wachambuzi wanasema bado itapitishwa.

Canada kwa upande yake nayo inamesa kuwa imetoa msaada wa  dola milioni 2.5 kwa umoja wa mataifa kusaidia shirika hilo kuangazia matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.