Pata taarifa kuu

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov anazuru Algeria.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov, anafanya ziara nchini  Algeria, taifa lenye utajiri wa gesi barani Afrika kwa mazungumzo na uwongozi wa taifa hilo , hii ikionekana kama njia ya serikali ya Moscow kutafuta njia mbadala na wasambazaji wapya wa bidhaa hiyo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi ,Sergei Lavrov.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi ,Sergei Lavrov. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Lavrov, aliwasili nchini Algeria siku ya jumatatu ambapo anatarajiwa kufanya kikao na waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo Ramtane Lamamra pamoja na rais Abdelmadjid Tebboune.

Hii ni zaira ya kwanza kwa afisa huyo wa ngazi ya juu katika serikali ya Urusi tangu mwaka wa 2019, ziara inayokuja pia wakati huu mataifa haya mawili yanapoaadhimisha miaka 60 tangu kuwanza kwa uhusiano wa kidplomasia kati yake.

Mwezi uliopita Rais wa Urusi Vladimir Putin, alifanya mazungumzo ya njia ya simu na mwenzake wa Algeria ambapo walijadili maswala mbalimbali ikiwemo ushirikiano wa OPEC+ na hali inayoendelea nchini Ukraine.

Algeria ni msambazaji mkubwa wa gesi barani Ulaya nchi za Italia, Hispania pamoja na mataifa mengine ya bara hilo yamekuwa yakitaka kufanya baishara na Algeria haswa wakati huu yakiwa mbioni kutafuta mshirika mwengine wa usambazaji gesi tangu Urusi kuivamia Ukraine feburuari 24.

Wachambuzi wa maswala ya uchumi wanaeleza kuwa Algeria haina uwezo wa kusambaza gesi kwa kiasi kikubwa barani ulaya haswa kwa kipindi hiki kifupi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.