Pata taarifa kuu

Vita Ukraine: Moscow yadai kuwa mazungumzo ya Istanbul yalikuwa "muhimu"

Duru mpya ya mazungumzo 'muhimu' imefanyika Jumanne huko Istanbul, kulingana na Moscow, ambayo imeahidi "kwa kiasi kikubwa" kupunguza shughuli zake za kijeshi katika mikoa ya Kyiv na Cherniguiv. Kwa upande wake, Ukraine inaomba makubaliano ya kimataifa ya kuhakikisha usalama wake.

Mazungumzo yalimalizika baada ya majadiliano ya saa 4 mjini Istanbul, Jumanne Machi 29, 2022.
Mazungumzo yalimalizika baada ya majadiliano ya saa 4 mjini Istanbul, Jumanne Machi 29, 2022. © Présidence turque / AP
Matangazo ya kibiashara

Awali pande zote mbili zilisema Jumatatu hazitarajii mafanikio makubwa.

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan amewaambia wajumbe kutoka Ukraine na Urusi kuwa maendeleo katika mazungumzo hayo yatafungua njia kwa mkutano mwengine kati ya viongozi wa nchi hizo mbili- Rais Volodymyr Zelensky na Rais Vladimir Putin.

Hayo yanajiri wakati takriban watu 5,000 wanaripotiwa kuuawa huko Mariupol, mji uliozingirwa na majeshi ya Urusi kwa wiki kadhaa, kulingana na afisa wa Ukraine. Umoja wa Mataifa unatafuta kufikiwa kwa "maelewano ya kusitisha mapigano" ili kuruhusu misaada kufafiki walengwa. Wakati huo huo zoezi la kuwahamisha raia limeanza tena, lakini mji wa Mykolaiv umekumbwa na mashambulizi ya anga ya jeshi la Urusi.

Katika hatua nyingine Mamlaka ya Ukraine ilisema siku ya Jumatatu kwamba walikuwa wameuteka mji wa Irpin, katika vitongoji vya Kyiv. Vikosi vya Ukraine pia vimezuia mashambulizi ya Urusi kuelekea Brovary, mashariki mwa Kyiv, katika muda wa saa 24 zilizopita.

Mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner wametumwa mashariki mwa Ukraine, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumatatu, ambayo inakadiria kuwa zaidi ya wapiganaji 1,000 kutoka kwa kampuni ya mamluki ya Wagner wanaweza kuletwa kupigana nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.